MAKINDA: SENSA ITATOA DIRA YA MAENDELEO

 


📌RHODA SIMBA

KAMISAA   wa Sensa  Tanzania bara na Spika  wa bunge msatafu  Anne Makinda amesema kuwa utekelezaji wa sensa ya watu na makazi ya  mwaka 2022 umeelekeza nguvu katika ngazi ya chini lengo likiwa ni kufanikiwa zaidi kwa kuwa sensa hiyo ndiyo inayotoa dira ya kupanga maendeleo ya nchi.

Ameyasema  hayo  leo Mei,24,2022 jijini hapa, wakati akifungua mkutano wa Wadau na Mashirika yasiyo ya kiserikali uliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),ili kujadili namna ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi  ambapo amesema kuwa serikali imeweka mkazo kwa sensa hiyo kwa kuimarisha  ili iweze kufanikiwa.

Amesema kuwa  sensa hiyo itafanikiwa endepo Mashirika na wadau watatilia mkazo katika utoaji elimu na uhamasishaji kwa wananchi ili wawe  na uelewa wa kuhesabiwa.

Serikali inaamini kutokana na upana wa mashirika yasiyo ya kiserikali yana uwezo wa kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi. Mashirika haya yamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli za wadau

Naye Mtakwimu Mkuu wa wa serikalk Dk. Albina chuwa amesema kuwa serikali haiwwzi kupanga maendeleo bila kuwa na idadi ya inayofahamika.

"Hii ni sensa ambayo inaenda kutupa hali halisi ya mwelekeo wa maendeleo. Pia sensa ya mwaka huu inaenda kuungana na ya majengo tutafahamu mazingira ya watu wabaishi vipi," amesema Dk. Chuwa.

Ameongeza kuwa suala la takwimu ni la ushirikishwaji wa watu wote hivyo ndio maana zaidi ya Mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi 7000 yameshirikishwa ili yakatoe elimu kwa wananchi.

Awali Mwenyekiti wa baraza la mashirika hayo Dk. Lilian Badi amesema kuwa ofisi ya takwimu imeelekeza nguvu nyingi katika kutoa elimu pamoja na kushirikisha Umma kuunga mkono katika zoezi la hilo ambalo linatarajiwa kuanza Agosti 23 mwaka huu.

Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa nchi ina Asasi zisizo za kiserikali ambazo zinaundwa na makundi mbalimbali ambayo zaidi ya 700 yamesajiliwa na yanafanya kazi.

" Sisi kama mabaraza tupo wajumbe 30 ambao tunawakilisha mashirika haya 733 yasiyo ya kiserikali, " amesema Mwenyekiti huyo.

Ameongeza kuwa wamejipanga kutumia mitandao yote ya kitaifa yote, makundi ya kijamii na mtu mmoja mmoja wanaoguswa na kazi za Mashirika hayo.

 

Post a Comment

0 Comments