NBS YAKANUSHA KUHUSIKA NA TANGAZO LA ORODHA YA KAZI ZA MAKARANI WA SENSA


📌RHODA SIMBA

OFISI ya Taifa ya Takwimu  (NBS) imekanusha taarifa zinazosambaa  katika  mitandao ya kijamii  kuhusu kutoka orodha ya majina ya makarani na wasimamizi wa sensa ya watu na makazi ikisema orodha hiyo siyo ya kweli na bado mchakato wa kupitia maombi bado unaendelea.  .

Taarifa hiyo imetolewa Leo Mei 27 jijini  hapa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema taarifa hizo siyo rasmi kwa watanzania waliyo omba nafasi za ukarani na usimamizi wa Sensa katika maeneo wanayoishi.

Dkt.Chuwa amesema muda wa maombi kwa nafasi hizo za kazi ulifika tamati tarehe 19 Mei ambapo idadi ya waombaji ilifikia 689,935 kati ya 205,000 wanaohitajika kwenye zoezi la sensa kwa mwaka 2022.

Watu hawa ambao hawana nia nzuri kwa Serikali na watanzania kwa ujumla wamekwenda  mbali na kutamka tarehe ya usahili kuwa ni 29  Mei 2022, napenda ifahamike kwamba mchakato  wa ajira  za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa bado unaendelea katika ngazi ya kata, shehia na Halmshauri zote
Dkt Chuwa.

Amesema  zoezi la uchambuzi wa maombi kwa waombaji wote linatarajiwa kuanza tarehe 02 Juni 2022 kwenye Kila kata au  shehia husika baada ya kukamilika kwa  mafunzo ya maafisa watakaohusika kufanya usahili.

Mchakato  wa ajira za makarani na wasimamizi wa sensa linakwenda vizuri kulingana na ratiba ya sensa
Dkt Chuwa

Hata hivyoo Dk Chuwa amewataka wananchi  kwamba taarifa yoyote  kuhusu mwenendo wa maandalizi ya sensa  ya watu na makazi  sensa ya majengo  na sensa ya anwani za makazi ikiwemo ajira  za muda zitatolewa   na Serikali kupitia vyombo vya habari.


Post a Comment

0 Comments