DKT JAFO:TANZANIA IMEPIGA HATUA MAPAMBANO MABADILIKO TABIA NCHI

 


📌RHODA SIMBA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi kupitia miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ikiwa ni jitihada za kupunguza uzalishaji wa gesi joto.

 Dkt. Jafo ameyasema hayo leo Mei 31, 2022 wakati wakati akizungumza na Jumuiya ya wanafunzi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani.

 Amesema pamoja na ukweli kwamba Tanzania siyo miongoni mwa nchi zinazozalisha gesi joto kwa wingi duniani, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imechukua hatua za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zikiwemo kujenga uwezo wa kitaasisi, kutoa elimu kwa jamii na; kuhimiza shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi. 

Amesema Tanzania pia imechukua hatua stahiki zikiwemo Kuandaa Mpango wa Taifa wa Kupunguza Gesijoto (2021 - 2026); Kuimarisha usimamizi wa misitu na program za upandaji miti; kuendelea na ujenzi wa Mradi wa umeme wa Bwawa la Mwl. Nyerere; Ujenzi wa Reli ya kisasa; kuanza kutumika kwa gesi majumbani na kwenye uendeshaji wa mitambo viwandani na kwenye magari badala ya dizeli na petroli na Matumizi ya mabasi yaendayo kwa kasi katika jiji la Dar es salaam.

 

Sisi tunaungana na Jumuiya ya Kimataifa kupunguza uzalishaji wa gesijoto, Tanzania pia imechukua hatua stahiki zikiwemo Kuandaa Mpango wa Taifa wa Kupunguza Gesijoto (2021 - 2026); tunatekeleza agenda ya mazingira kwa vitendo” Dkt. Jafo alisisitiza.

 Akiwa chuoni hapo Dkt. Jafo ametoa pongezi kwa Chuo cha Mipango kwa kuwa mstari wa mbele kusukuma mbele agenda ya mazingira kwa vitendo kwa kuwa mstari wa mbele katika upandaji miti na kuhamasisha utenganishaji wa taka na kuzitumia kwa matumizi mengine.

Niwaponge kwa kutunza mazingira, Dodoma ni ardhi kame ila ukifika hapa ni kama uko mbinga, miti ni mingi na inapendeza sana
Dkt. Jafo

Akitoa taarifa ya usimamizi wa Mazingira Chuoni hapo, Mkuu wa Chuo cha Mipango Prof. Hozen Mayaya amesema Chuo hicho kinaongoza kwa kutoa kozi na wahitimu waliobobea katika masuala ya Mazingira nchini na kuteleleza miradi ya urejeshaji taka na upandaji miti.

Kuelekea Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu shughuli mbalimbali za hifadhi na usafi wa mazingira zinazofanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma zikuhusisha wananchi, taasisi, mashule, vyuo na viongozi mbalimbali ambapo kaulimbiu ya kitaifa inayoongoza maadhimisho haya ni ”Tanzania ni moja tu: Tutunze Mazingira”

Post a Comment

0 Comments