RAIS MWINYI KUFUNGUA WIKI YA UBUNIFU DODOMA

 


📌RHODA SIMBA

RAIS na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kufungua maadhimisho ya wiki ya Ubunifu na mashindano ya kitaifa ya sayansi,Teknolojia na ubunifu(MAKISATU) Jijini Dodoma mnamo tarehe 16 Mai mwaka huu.

Wiki ya kitaifa ya ubunifu ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya awamu ya 6 yenye lengo la kuongeza hamasa ya matumizi ya sayansi,Teknolojia na ubunifu kama nyenzo ya kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii.

Akizungumza Jijini Dodoma Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Aldof Mkenda amesema kuwa maadhimisho ya wiki ya ubunifu yatafanyika katika ngazi ya mikoa na Taifa.

Aidha amewataka watanzania kuendelea kutumia bunifu mbalimbali za kitanzania katika shughuli za maendeleo ya kijamii Ili kukuza na kuendeleza bunifu na Teknolojia.

Natoa rai kwa watanzania kuendelea kutumia bunifu mbalimbali za kitanzania Katika shughuli za Maendeleo ya kijamii na kiuchumi ili kukuza  na kuendelea  bunifu na Teknolojia hizi.
Waziri Mkenda.

Sambamba na hilo amesema Maadhimisho ya wiki ya ubunifu yatafanyika katika ngazi ya mikoa na Taifa ambapo katika ngazi ya mikoa maadhimisho haya yanaratibiwa kwa ushirikiano Kati ya Wizara ya Elimu,sayansi na Teknolojia,Tume ya sayansi na Teknolojia(COSTECH) na program ya FUNGUO chini ya UNDP kupitia kumbi za ubunifu na Vituo vya ubunifu,taasisi za Umma na binafsi katika mikoa husika,Aidha Uratibu huo unahusisha OR-TAMISEMI kupitia Maafisa maendeleo ya jamii.

Aidha Prof.Mkenda ameleza kuwa katika ngazi zote mbili mikoa na Taifa maadhimisho ya wiki ya ubunifu yanaambatana na matukio mbalimbali ikiwemo kilele Cha MAKISATU yanayolenga kupata washindi kwa mwaka 2022 katika ngazi ya kitaifa,


 

Kadhalika amesema kuwa maadhimisho ya wiki ya ubunifu na MAKISATU yanalenga pamoja na mambo mengine ni kuibua,kutambua na kuendeleza jitihada zinazofanywa na wabunifu wa kitanzania na kuhamasisha matumizi ya sayansi,Teknolojia na ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Amesema kuwa maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya ubunifu yanatoa fursa kwa wabunifu/wagunduzi kujitangaza na kujulikana kwa wawekezaji,watumiaji wa bidhaa zao na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi.

Mikoa iliyofanikiwa kuandaa maadhimisho ya wiki ya ubunifu kwa mwaka huu ni pamoja na Dar es Salaam,Dodoma,Mbeya,Arusha,Iringa,Mwanza,Zanzibar,Tanga,Kilimanjaro,Morogoro,,Njombe,Kagera ,Mtwara,Kigoma,Mara na Ruvuma,ngazi ya mikoa maadhimisho hayo yalianza tarehe 27 Aprili mwaka huu na yanatarajiwa kukamilika tarehe 12 Mei.

Prof.Mkenda

Aidha amesema kuwa katika ngazi ya taifa maadhimisho ya wiki ya ubunifu yatafanyika kuanzia tarehe 12 Hadi 20 mei mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri.

Hafla ya kufunga itafanyika tarehe 19 Mei mwaka huu na itaambana na utoaji wa tuzo mbalimbali kwa washindi wa MAKISATU,washiriki wa maonyesho na wadau mbalimbali na mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt.Philip Isdori Mpango.

 

Post a Comment

0 Comments