SERIKALI KUWEKA UTARATIBU WA KUTOA ELIMU KWA WATUMISHI KUHUSU KANUNI MPYA YA MAFAO YA PENSHENI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA 

SERIKALI imeweka utaratibu wa kutoa elimu kwa watumishi wa  Umma  kuhusu kanuni mpya  ya mafao ya pensheni  kwa wastaafu kwa lengo la kuhakikisha  wote wanakuwa na uelewa sahihi juu ya kanuni hiyo huku ikitangaza kiwango kipya cha kikokotoo cha mafao ya mkupuo sasa ni asilimia 33 kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii.

Hayo yamesemwa leo Mei 26 jijini hapa na katibu  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Prof.Jamal Katundu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa hatua  imefikiwa baada ya makubaliano kati ya serikali,chama cha waaajiri nchini(ATE) na shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA baada ya kusitishwa kwa kanuni zilizotengenezwa Disemba 28 mwaka 2018.

Katibu huyo amesema kuwa wamekubaliana kikokotoo limbikizi kitakuwa 1/580 kama ilivyokuwa kwa mfumo wa hifadhi ya jamii NSSF na ilikuwa mifuko ya PPF,GEPF na baadhi ya wanachama wa iliyokuwa PSPF na LAPF.

Amesema kuwa Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ya masuala ya hifadhi ya jamii ilitunga kanuni za mafao zilizolenga kutumika kwa wanachama na wategemezi wanaostahili kwa mafao yote mawili.

"Kanuni za mwaka 2018 zililalamikiwa na baadhi ya wadau hivyo Serikali ilisitisha utekelezaji wake tarehe 28 disemba 2018 na kuelekeza kanuni zote za mafao zilizokuwa zinatumika katika mifumo iliyounganishwa ziendelee kutumika katika kipindi Cha mpito wadau husika(Serikali,waajiri na wafanyakazi)wakae na kukubaliana kanuni itakayowianisha mafao kwa wafanyakazi wote,"amesema 

Aidha amesema kuwa mwaka 2018 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma Na.2 ya mwaka 2018.

Amesema sheria hiyo iliunganisha mifuko ya GEPF,LAPF,PPF na PSPF kuwa Mfuko mmoja wa PSSSF kwa lengo la kutoa mafao Bora na kufanya Mfuko mpya kuwa endelevu,pia sheria hiyo ilifanya mabadiliko ya sheria ya Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii(NSSF) na kufanya kuwa Mfuko rasmi wa kuwahudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

"Pamoja na mambo mengine kamati hii ilipewa jukumu la kuishauri Serikali kanuni itakayotumika baada ya kipindi Cha mpito itakayozingatia maslahi ya wafanyakazi na uendelevu wa mifuko,

Pamoja na kamati elekezi iliundwa kamati ya wataalamu kutoka katika Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali,chama Cha waajiri na Shirikisho la vyama vya wafanyakazi,kamati hii ilikuwa na jukumu la kuandaa na kuchambua nyaraka mbalimbali kwaajili ya kuishauri kamati katika kutekeleza Mpango Mkakati wa kipindi Cha mpito,"amesisitiza.

Kadhalika amesema kuwa kamati elekezi ilifanya kazi yake kwa kuzingatia Mambo makuu mawili ambayo ni kuhakikisha kanuni inayopendekezwa inatoa mafao Bora kwa wastaafu na kanuni mpya inahakikisha kuwa mifuko yote inakuwa endelevu kwa Manufaa ya wanachama wote.

 

 

 

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments