SERIKALI NA USAID KUBORESHA MAPAMBANO VIFO VYA MAMA NA MTOTO

 


📌RHODA SIMBA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele katika kuboresha  huduma za afya ili kupambana na vifo vya mama na mtoto.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Mei 6 jijini hapa wakati akizindua mradi wa Afya Yangu unaotekelezwa hapa nchini kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) kwa miaka mitano.

Amesema katika kutekeleza hilo Serikali ilianza na kuboresha vituo vya afya ambapo  hadi kufikia mwaka 2020 vituo 487 vya afya  vilikuwa vimejengwa na hospitali za wilaya 102 zimejengwa na kukarabatiwa


Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na wadau wamefanya jitihada kubwa katika kuhakikisha maambukizi ya virusi vya ukimwi yanapungua nchini ambapo jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda.

Amesema jitihada za kupunguza maambukizi ya virusi zimezaa matunda kwani maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto imeshuka kutoka asilimia 13.5  hadi kufikia asilimia 7.

Hadi kufikia Disemba mwaka jana asilimia 89 ya watu   walikuwa wanatambua hali yao ya maambukizi huku asilimia 85.5 ya watu wanaoishi na maambukizi ya vurusi vya ukimwi walikuwa kwenye dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo hayo ni maendeleo makubwa yanatokana na utendaji wa serikali  pamoja na wadau

Amesema serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele katika kupambana na vifo vya mama na mtoto.

“Tunampongeza Rais Samia kwa dhamira yake ya kuboresha huduma za afya kuanzia ngazi za vijiji na awapongeza USAID tawi la Tanzania  kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhimarisha huduma za afya  kwa utekelezaji wa afua za  kifua kikuu,ukimwi,uzazi wa mpango na maambukii ya ukimwi,”amesema


 

Kwa upande wake Waziri wa Aya Ummy Mwalimu alisema  mradi huo inaozinduliwa utatekelezwa katika mikoa 21 ya Tanzania bara  na utagharimu sh,billion 596 .

Waziri Ummy amesema serikali inatambua mchango wa wadau wa afya katikakuhimarisha utoaji wa huduma za afya bora na mahitaji ya sekta ya afya ni makubwa nchini hivyo ni muhimu wadau wakaendelea kuunga mkono jitihada za serikali.

Sisi kama serikali kupitia Wizara ya Afya tunawahakikishia kuwa tutaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwepo na ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma za afya na kama kuna changamoto tupo tayari kuzifanyia kazi

Amesema kama Wizara ya Afya wamejitathmini na kipaumbele kikubwa wataelekeza katika ubora wa huduma za afya na takwimu kwa mwaka huu zinaonyesha kuwa katika wamama 100 wajawazito 99 walihudhuria kliniki je tunakuaje na  watoto wanazaliwa na virusi vya ukimwi

 


Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shiirika la Marekani la Maendeleo ya kimataifa(USAID)  Kate Somvongsiri amesema takwimu zinonyesha kuwa Zaidi ya watu milioni 1.7 wanaishi na virusi vya ukimwi nchini Tanzania.

Amesema kazi kubwa inatakiwa kufanyika ili kupunguza  idadi ya watoto wanaozaliwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi ikiwemo kutekeleza afua mbalimbali ambazo zitasaidia kupunguza hali hiyo

“Tunaipongeza serikali ya Tanzania na wizara ya afya kwa ushirikiano tunaopata katika kutekeleza miradi mbalimbali inayohusu afya za wananchi wake na katika mpango kazi huu wa miaka mitano tumejipanga na tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali itakayoleta tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla,”amesema 


 

Awali akitoa salamu za Mkoa Mkuu wa Mkoa wa   Dodoma Antony Mtaka alitumia fursa hiyo kuyakaribisha mashirika na taasisi za kimataifa ambazo bado hazijapata ofisi katika mkoa huo kufika ofisini kwake kwaajili ya kupata ardhi ili wajenge ofisi.

“Natumia fursa hii kuwakaribisha Dodoma makao makuu ya nchi na kwa mashirika ambayo hayajapata ofisi wafike ofisi tutawapa ardhi ili wajenge ofisi zao hapa yalipo makao makuu ya nchi na serikali,”amesema Mtaka

 

Post a Comment

0 Comments