WAZIRI SIMBACHAWENE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ALGERIA

 


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria nchini Tanzania Mhe. Ahmed Djellal alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mei 31, 2022 Jijini Dodoma.


Katika mazungumzo hayo masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo kudumisha ushirikiano bana ya Tanzania na Algeria katika kuhakikisha ustawi wa Nchi zote mbili pamoja na raia wake.

Balozi wa Algeria alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji nchini huku akiahidi kutoa ushirikiano katika kuimarisha mahusiano yaliyopo.


 

 

Post a Comment

0 Comments