CCM YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUFANYA MARIDHIANO NA VYAMA VYA SIASA

 

📌RHODA SIMBA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu  Hassan kwa  kufanya  maridhiano na vyama vya siasa  nchini kwa lengo la kuimarisha  umoja  ushirikiano  mshikamano  amani na utulivu kwa maendeleo na ustawi  wa watanzania  wote.

Hayo yamesemwa leo June 22 jijini hapa na Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka  wakati akitoa mrejesho mara baada ya kumalizika kwa kikao cha  Halmashauri kuu ya  taifa  ya chama cha mapinduzi.

Amesema Chama Cha Mapinduzi kimeishauri Serikali kuharakisha utekelezaji wa  masuala  yote  yatakayojenga  kuaminika, kuimarisha  ushirikiano na umoja  wa kitaifa kwa ustawi wa wananchi wote.

“kama ambavyo mnafahamu wiki 3 zilizopita chama cha mapinduzi kipo kwenye mazungumzo ama majadiliano,maridhiano na Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA) ninayofuraha kuwajulisha kwamba mazungumzo hayo yanakwenda vizuri na hivi ninavyowaambia leo halmashauri kuu ya taifa imepokea taarifa ya mazungumzo hayo ambayo kwa upande wa CCM tumekuwa tukishiriki hatua zote kuhakikisha dhamira na dira na msimamo wa Mheshimiwa Rais kwenye kusimamia jambo hilo linatimia,

Tayari vikao viwili vimeshakaa upande wa Chama Cha mapinduzi na upande wa chadema tumekutana pamoja na mazungumzo yanakwenda vizuri sasa kwenye hayo mazungumzo CCM tunaishauri ama tunaiomba serikali iangalie namna ambavyo inaweza ikaangalia kesi zile za wanachama ama zakisiasa ambazo ziko kwenye vyombo mbalimbali vya kisheria kwa mujibu wa katiba ya nchi lakini kuona namna nzuri ambavyo wanaweza wakamaliza kwa haraka zaidi kesi hizo za kisiasa ama wale ambao wanakabiliwa na tuhuma hizo za kisiasa basi Serikali ione namna nzuri ya kumaliza kwa nia nzuri,”amesema Shaka.

Aidha amesema kuwa mfano uliooneshwa na Rais Samia ni lazima uungwe mkono na  halmashauri kuu ya Taifa imeunga mkono msimamo wa Rais Samia na katika  hilo wamehakikisha kwamba vyama vyote vya siasa CCM itaendelea kuimarisha Demokrasia nchini.

Amesema kuwa CCM itaendelea kuimarisha demokrasia bila kuathiri amani,umoja na mshikamano wa taifa,na kwamba vyama vya siasa vitaendelea kutoa ushirikiano kwa Chama Cha Mapinduzi.

“Jambo kubwa ambalo ningependa nizungumze kwenu Chama Cha Mapinduzi tunasisitiza umuhimu wa uwepo wa katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na kuona namna bora ya kufufua,kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa maslahi mapana ya taifa na maendeleo kwa ujumla,”amesema shaka.

Amesisitiza kuwa vyombo vya habari vinayo nafasi ya kuwa sehemu ya kuelimisha maridhiano hayo ya kisiasa ambayo yanakwenda vizuri,kwani maridhianoa hayo hayatawahusu wanasiasa pekee bali hata jamii kwa ujumla.

Hata hivyo kabla ya kikao cha Halmashauri kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kuketi jana june 21 kulifanyika kikao cha kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM pamoja na kikao cha siku moja cha kawaida ambacho kiliongozwa na mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Post a Comment

0 Comments