DKT.YONAZI AWATAKA MAWASILIANO KUWA CHACHU YA UCHUMI SHINDANI WA KIDIJITALI

 


📌RHODA SIMBA


KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi amewataka wafanyakazi wa sekta ya Mawasiliano nchini kukuza maarifa na kuwa na uchumi shindani wa kidijitali ili kuwa kitovu cha watu kujifunza namna ya kutafuta fursa katika taasisi za kimataifa.

Akizungumzia  leo June 21  jijini Dodoma katika kikao kazi cha uchambuzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya Mawasiliano kitaifa na kimataifa Jimmy Yonazi amesema kuwa Wizara ya Mawasiliano imekusudia kufungua ajira kwa watanzania kitaifa na kimataifa ili kuwa nchi yenye fursa nyingi lengo likiwa nchi zingine nazo zije kujifunza hapa nchini.

Lengo letu ni kufungua ajira kwa watanzania kitaifa na kimataifa Ili kuwa na nchi yenye fursa nyingi Ili nao watu wa mataifa wengine  waje wajifunze kutoka hapa mchini kwetu
Dkt.Yonazi

Aidha Yonazi amesema kila mmoja atambue jukumu lake siyo kuja ofisini na kurudi nyumbani tu ambapo amewasisitiza kufanya kazi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kimataifa.

"Kila mmoja akitambua jukumu lake amekuja hapa kufanya nini tutapiga hatua  hata kwa mataifa mengine"amesema Yonazi

Kwa upande wake mkurugenzi wa TEHAMA Kutoka  Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku amesema kuwa watatekeleza maagizo ya Serikali ili kuongeza ajira pamoja na pato la Taifa.

"Tutaenda kutekeleza yale tuliyoelekezwa na Serikali na   niseme tu tutafanya kwa weledi ili kuhakikisha ajira na Pato la Taifa  linaongezeka" amesema Munaku.


 

Post a Comment

0 Comments