CHONGOLO ATOA WITO NGAZI ZOTE ZIWEKEZE KWENYE UCHUMI.

 


📌RHODA SIMBA

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimetoa wito kwa ngazi zote za Watendaji kuanzia Tawi, Kata, Wilaya na Mikoa yote Nchini kuwekeza nguvu kwenye uwekezaji na utendaji wa uchumi wa chama.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo katika Kongamano la Mafunzo ya Uongozi na uwajibikaji katika mada za Itikadi, Elimu ya Sensa na makazi,Tehama na Usajili wa Wanachama pamoja na Masuala ya Ulinzi na Usalama kwa Viongozi wa Chama kuanzia ngazi za Mashina Jijini Dodoma.

Chongolo amesema uboreshwaji wa uchumi kwenye chama itasaidia mambo yote kuwa rahisi na wataepuka kukimbiana katika vikao vya kujenga masuala yote ya msingi.

Ni lazima kwanza tuboresha uchumi ili mambo yatunyookee, tukiboresha uchumi wa chama chetu mambo yetu yote yatakuwa rahisi na tutaacha kukimbiana kwenye masuala ya Msingi,

Na hivi karibuni tutakusanya mikoa ambayo imelala lala tunawachukua waje kujifunza waone Mikoa mingine inavyofanya vizuri Mkoa wa Dodoma ni moja kati ya Mikoa inayofanya vizuri katika suala la Uchumi.

Chongolo.

Aidha amesisitiza kwa wagombea kuepuka suala zima la rushwa katika kipindi hiki cha uchaguzi ikiwi ni kiapo cha Mwanachama ambapo ni ahadi katika chama.

Tunaposoma ahadi ya Mwananchama kila Mmoja aliapa kuwa rushwa ni adui wa haki na pale mlikuwa mkimaanisha kuwa rushwa ni jambo lisilokubalika,kila Mmoja atumie yale mema yake ambayo anaona ataweza kujinadi

Tufanye Kampeni kwa kutumia nguvu zetu bila kutengenezeana uongo na uzushi pamoja na kutengenezeana ajali tusipende kuwekeana chuki sisi kwa sisi

Aidha Chongolo aliagiza vikao vitakavyo jadili majina ya wahusika katika ngazi husika kutoona aibu kuchukua hatua kwa watu watakaokiuka maagizo halali yaliyowekwa na Chama.

Hatuwezi kuwa chama ambacho tunatoa maelekezo kwaajili ya kutoa fursa kwa watu wote kuwa sawa kwenye kugombania kinyang'anyiro cha kugombea nafasi mbali mbali na baadhi ya wachache kuona wao wanapembe ndefu kuliko mmiliki wa pembe husika

Chama ndicho chenye dhamana na nafasi, Mtu ukiona unataka dhamana hiyo usipofuata maagizo na maelekezo yetu utakuwa hututakii jambo zuri na utakuwa unatulazimisha kuchukua hatua na hatutosita kuchukua kwasababu utakuwa ameyataka mwenyewe. 

Chongolo

Kadhalika amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwasababu ndio nyenzo ya msingi ya kuwezesha kutekeleza majukumu kwa miaka 5.

Kwenye mafunzo hayo yapo mambo ambayo yatatolewa kwaajili ya wakati likiwemo suala la Sensa ambalo tumepata bahati yakupata makamishina wa sensa Tanzania kuja kuzungumza sensa kwaajili ya uelewa wetu lakini na sisi wote kuwa wakufunzi wa wenzetu kule tulipotoka ili zoezi la sensa wakati ukifika lifanyike kwa ufanisi mkubwa na kiwango cha hali ya juu,"amesema Chongolo.

Pia amesisitiza kuwa sensa ni uchumi,sensa ni maendeleo na sensa ndio kila kitu kwani bila kujua idadi hakutakuwa na mipango ya maendeleo.

Amesema kuwa katika Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ukiangalia fungu la 3 ukurasa wa 15 wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi toleo la mwaka 2022 inaeleza ngazi ya msingi ya uongozi wa Chama na ngazi hiyo imetaja wazi kwamba ni ngazi ya shina.

Kwetu sisi thamani ya balozi haielezeki na Wala haina mjadala ni ngazi ya msingi na ni kiongozi mwenye heshima ndani ya Chama chetu,kwani ndiye kiongozi anayejishighulisha na masuala ya wananchi moja kwa moja ndio maana kwa heshima hiyo balozi pekeee ndiye amepewa dhamana hata ya kupeperusha bendera kwa saa24 tofauti hata na Katibu Mkuu wa Chama hicho wala haina mjadala katika hilo

Naye Naibu Katibu Mkuu CCM bara Christina Mndeme amesema kuwa tarehe 23/08 katika zoezi la sensa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ibara ya 206 kifungu Cha 1 kifungu kidogo cha i-iii alisema CCM kupitia Ilani yake ya mwaka 2020-25 waliahidi kuwa na takwimu sahihi za watu na makazi.

Kuwa na takwimu sahihi za viwanda na biashara,kuwa na takwimu sahihi za kufahamu nguvu kazi ya taifa, kwahiyo jambo hili ambalo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ametuonesha njia na amelipa ridhaa na amelipa baraka zote ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi

Hivyo ni wajibu wenu kila mmoja kwenda kulitekeleza hili kwa vitendo na kuhamasisha watu wajitokeze kuhesabiwa kwani sisi mabalozi na wenyeviti wa matawi, mashina ndio tunaishi na wanachini ndio tunafahamu nani anakaa wapi, ana wageni wangapi, wanaishi wangapi hili zoezi tukalisimamie

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesema kuwa Serikali haina mgogoro wowote na chama kuanzia ngazi ya Wilaya mpaka Mkoa na kuahidi kuwa hawatarudi nyuma kwani wanafurahishwa na namna Chama Cha Mapinduzi kinavyofanya kazi

Aidha amesema kuwa katika kuelekea kwenye uchaguzi kutoka kwenye matawi, kata, Wilaya na Mkoa ameshazungumza na Wakuu wa Wilaya ili kuhakikisha hawaingilii uchaguzi wa ndani ya Chama na kuwasihi viongozi wa Serikali kutojihusisha na uchaguzi lakini wako tayari kufanyakazi na kiongozi yeyote atakayechaguliwa.

 

Post a Comment

0 Comments