DUWASA YAJIPANGA KUHAKIKISHA WAKAZI WA JIJI LA DODOMA WANAPATA MAJI.

 

📌RHODA SIMBA

IMEELEZWA kuwa ili kuhakikisha wakazi wa Jiji la Dodoma wanapata maji safi na salama, serikali inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mradi wa kutoa maji kutoka bwawa la Mtera unaotarajiwa kutekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 326.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) wakati akieleza utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 mbele ya waandishi wa habari.

Ujenzi wa Mradi wa kutoa maji Bwawa la Mtera Chanzo tayari kipo kitakamilishwa kati ya miaka (2 – 2.5) Benki ya Dunia ipo tayari kufadhili na Gharama ya Mradi ni Dola milioni 140 (326bn) Utaongeza maji lita milioni 130 kwa siku, Utaongeza mtandao wa usambazaji maji katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na kuondoa mgao wa maji.

Aidha Mhandisi Aron amesema Mradi huu utahusisha ujenzi wa mabwawa 16 eneo la Nzuguni Utaongeza mtandao wa majitaka usiopungua kilomita 250 na mradi utaunganisha wateja wasiopungua 6,000 pia Utaongeza huduma ya usafi wa Mazingira kutoka asilimia 20 hadi 45. Mradi una gharama ya Tsh. 161bn. 

Mradi upo katika hatua za mwisho za kumpata Mkandarasi Mshauri na Mradi wa Majitaka na uboreshaji huduma ya Majisafi kwenye Mji wa Serikali 

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na DUWASA ipo katika hatua za mwisho kusaini mkataba na Mhandisi Mshauri. 

Mradi huu unatarajiwa kugharimu takribani shilingi za Tanzania Bil. 94, ambazo zimeshatengwa na Serikali Kuu.

Pia Mhandisi Aron amewataka wananchi kutunza miundombinu ya majisafi na majitaka Lakini pia kutunza vyanzo vya maji kwa kuboresha mazingira hasa upandaji na utunzaji wa miti.

Aliwataka wananchi kuwa na matumizi sahihi ya maji na kuhifadhi maji,Matumizi sahihi ya mtandao wa majitaka.

Pia naomba niwakumbushe wateja wote wa DUWASA kulipa Ankara zao kwa wakati ili kuzuia usumbufu wa kukatiwa maji

Mhandisi

 

 

Post a Comment

0 Comments