MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YAFIKIA ASILIMIA 87.

 

📌RHODA SIMBA

SERIKALI imesema maandalizi ya sensa ya watu na makazi yamefikia asilimia 87 ambapo kwa sasa imeanza kutoa mafunzo kwa wakufunzi wa sensa katika ngazi ya Mkoa.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Julai 6 Jijini Dodoma Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa amesema mafunzo hayo yatafanyika kwa siku 21 na yatahusisha wataalamu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, waratibu wa sensa ngazi ya wilaya,pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya watu wenye ulemavu.

Amesema baada ya mafunzo hayo washiriki watakaofaulu watakuwa na wajibu wa kwenda kufundisha wasimamizi na makarani wa sensa ambao watapata nafasi baada majina yao kutangazwa katika maeneo waliyoomba.

Hadi sasa zoezi la maandalizi linaenda vizuri, baada ya kukamilisha mafunzo ya wakufunzi katika ngazi ya Taifa hatua inayofuata ni mafunzo katika ngazi yaMikoa ambapo yameanza rasmi leo katika mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar na mafunzo haya yatafanyika kwa siku 21

Ameongeza kuwa"Baada ya kukamilika Kwa mafunzo hayo Julai 29 mwaka huu yatafuata mafunzo katika ngazi ya Wilaya ambapo kutakuwa na makarani,wasimamizi wa maudhui,na wasimamizi wa TEHAMA itahusisha  washiriki walioomba nafasi hizo na kukidhi vigezo na kufanya usahili.

Kwa mujibu wa Dk.Albina amesema katika tathmini ambayo wameifanya hivi karibuni wamebaini kuwa asilimia 97 ya wananchi wamekubali kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu

Amesema hiyo ni hatua kubwa ukilinganisha na mwaka 2012 katika kipindi kama hichi ni asilimia 80 ya wananchi ambao walikuwa wamekubali kuhesabiwa.

Tuko makini katika suala la Sensa tutahakikisha hadi kufikia siku ile ya Sensa tutakuwa tumekamilsha hatua zote zinazohitajika na kwasasa ukiangalia ratiba yetu imebana sana hatuna muda wa kupoteza

Kuhusu usiri wa taarifa zitakazokusanywa Dk Albina aliwatoa hofu wananchi kuwa sheria za takwimu zinaeleza kuwa kwa wasimamizi wa zoezi hilo watakaovujisha siri ni kifungo cha miaka miwili jela, au faini sh. milion 2 au vyote kwa pamoja

Amesema pia wasimamizi kabla ya kufanya zoezi hilo watapewa kiapo maalumu cha kutunza siri za watu.

Niwatoe hofu watanzania kuwa serikali imedhamilia kufanya zoezi hili kwa umakini mkubwa tutahakikisha kila kitu atakachokisema mwananchi inakuwa ni siri kati yake na karani na kwa atakayekiuka sheria itafuata mkondo wake

 

 

Post a Comment

0 Comments