MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI ATANGAZA KUANZA MAFUNZO YA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA.

 

📌RHODA SIMBA

MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa ametangaza kuanza kwa mafunzo kwa Makarani na Wasimamizi wa sensa 20,5000 waliopatikana baada michujo mbalimbali.

Dkt.Albina ameyasema hayo jijini Dodoma ambapo amesema mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza rasmi Julai 31 hadi Agosti 18 mwaka huu.

Amesema mchakato wa kuwapata watendaji hao wa muda ulienda vizuri na umefuata miongozo yote iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Baada ya kumalizika kwa mafunzo ya wakufunzi wa sensa sasa hatua inayofuata ni mafunzo kwa makarani na wasimamizi wa sensa ambao watafundishwa vizuri kuhusu kufanikisha tukio hili,na hapa nataka nisisitize kuwa kwa wasimamizi na makarani ambao watashindwa mitihani wataondolewa mapema na nafasi zao zitachukuliwa na watu wengine kwasababu tunayo hazina ya kutosha

Mtakwimu Mkuu.

Amesema kwa Makarani na Wasimamizi wa sensa watakaofuzu mafunzo watakuwa na wajibu wa kufika katika maeneo ya kuhesabia watu siku mbili kabla ya zoezi la kuhesabu kuanza kwa ajili ya kutambua mipaka ya eneo atakalofanyia kazi na kuhoji dodoso la kijamii.

Dk.Albina ametoa rai kwa Wasimamizi na Makarani wa sensa kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaotoa siri za taarifa watakazo kusanya kutoka kwa wananchi.

Amesema adhabu zipo kisheria na karani atakayetoa siri za mtu atalipa faini ya shilingi Milioni 2 au kifungo cha miezi 6 au vyote kwa pamoja.

Niwahakikishie wananchi kuwa taarifa watakazozitoa zitakuwa salama kwasababu hawa makarani na wasimamizi kabla ya kupangiwa vituo watapewa kiapo cha utii ambapo atakayekiuka sheria itafuata mkondo wake

 

Post a Comment

0 Comments