SERIKALI IMETOA VIFAA KAZI KWA VIJANA NCHINI VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 371.

 

📌RHODA SIMBA

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu imetoa vifaa vya kuanzia katika fani ya ushonaji uchomeleaji na utengenezaji wa vifaa vya aluminium kwa vijana 1741 wa mikoa 26 nchi nzima vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 371 .

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) leo jijini Dodoma, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi vijana ajira na watu wenye ulemavu Patrobass Katambi amesema vifaa hivyo ni pamoja na vifaa vya kushonea (cherehani) 400 seti 75 za uchomeleaji na uungaji vyuma pamoja na seti 70 ya uchomeleaji aluminium.

Vifaa hivi vinaenda kugawiwa kwa vijana lengo likiwa ni kuwawezesha kuhakikisha kwamba wanavitumia zaidi katika kujiajiri na kama mnavyofahamu Ofisi yetu inatekekeza miradi mbalimbali ya kuwawezesha vijana lakini tunawatumia TAMISEMI kwaasababu wao ndio wanaohusika na kuwapata vijana katika ngazi ya mtaa

Vijana wote wenye sifa za kupatiwa ni pamoja na vijana wenye ulemavu kupitia vyuo vya wenye ulemavu vijana wenye ulemavu kwenye vikundi vyao vijana waliojiunga kwenye shughuli za uchumi,vikundi vinavyorejesha mikopo kwa wakati katika halmshauri zao na vijana waliotayari kufanya shughuli za uchumi

 Katambi

Aidha amewataka vijana watakaopata fursa hiyo wakapate ushauri kutoka kwa wataalamu ili shughuli zao zikawe na tija sambamba na kuzitaka halmashauri kutoa tenda kwa vikundi vya vijana ili kuwakwamua kiuchumi na kupata faida itakayowawezesha kurejesha mikopo hiyo.

Kuliko kuwapa vijana fedha bila kuwapa elimu TAMISEMI na ofisi ya Waziri Mkuu itabidi tujipange ili kwenda kutoa elimu zaidi ili fedha itakayorejeshwa iwapatie watu wengine

Kwa upande wake Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Prof Jamal Katundu amesema lengo lakutoa vifaa hivyo nikuwezesha mchakato wa kutoa ajira kwa vijana.

Naye Mkurugenzi msaidizi idara ya serikali za mitaa (TAMISEMI) Humfrey Hilali amesema kuwa ugawaji wa vifaa hivyo unakamilisha dhana ya ugatukaji wa madaraka.

Akizungumza kwa niaba ya vikundi vya vijana Gladis Jamal ameishukuru Serikali ya awamu ya sita (6) kwa kuwapatia vifaa hivyo ambavyo vitaenda kuwasaidia kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.



 

Post a Comment

0 Comments