SHEKIMWERI APONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUHUDUMIA WANANCHI KUPITIA KAMPENI YA AFYA BOMBA

 

📌RHODA SIMBA

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri amelipongeza Jeshi la Polisi kupitia kituo cha afya Polisi Dodoma kwakujitoa kuhudumia wananchi kupitia kampeni ya afya bomba pima.

 Kampeni hiyo imeanza leo hadi Julai 31 ambapo wananchi wanapata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, figo, moyo, tezi dume, kinywa na meno pamoja na magonjwa ya kina mama.

Akitoa pongezi hizo, Shekimweri amesema mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 30 hiyo ikiwa inaashiria uzalendo kwa manufaa ya umma yenye tija.

Binafsi nimefurahishwa na nimeridhishwa kwamba mmefanya kazi hii kizalendo askari mmetekeleza mradi huu kizalendo. Askari mmetekeleza mradi huu kwa gharama nafuu mimi niwahakishie kwamba tupo tayari kuwaaunga mkono katika ajenda hii kubwa muhimu kwasababu mmeunga mkono jitihada za serikali katika kuwahudumia wananchi masuala ya afya. 

Shekimweri.

Ameongeza kuwa, serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 500 kwaajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Nala jijini Dodoma huku akiwasisitiza wananchi kijitokeza kuhesabiwa kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi.

 Natoa rai kwa wananchi jitokezeni kwa wingi moja kupima kwenye kituo cha polisi hapa Dodoma na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetupatia million 500 za kuanza kujenga kituo cha afya Nala na muhimu zaidi tujitokeze kuhesabiwa ili mipango ya maendeleo ikapangwe vizuri’amesema

Shekimweri 

Akisoma risala mtoa huduma wa kituo hicho Redemta Kisima ameelezea changamoto zinazokabili Kituo cha Afya polisi Dodoma kuwa ni uhaba wa majengo hususani jengo la kujifungulia wakina mama, madaktari bingwa na chumba cha upasuaji.

Tunazo changamoto chache zinazotukabili ikiwemo uhaba wa majengo hususani chumba cha kujifungulia, wodi ya wagonjwa mahututi, wodi ya watoto,wodi ya upasuaji, madaktari bingwa, madaktari wa upasuaji na madaktari wa watoto wauguzi wafamasia na wataalam wa maabara 

Kisima

 

 

Post a Comment

0 Comments