BILIONI 9.9/ZIMETENGWA KWA AJILI YA KUJENGA MAABARA DODOMA NA MWANZA.



📌 JASMINE SHAMWEPU

 JUMLA ya kiasi cha shilingi bilioni 9.9 imetengwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya kujenga jingo la maabara katika miji ya kimkakati Dodoma na Mwanza ili kusogeza huduma za shirika karibu kwa wateja na kuongeza ufanisi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Dk. Athuman Ngenya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya vipaumbele na mikakati yao katika mwaka wa fedha 2022/23.

Akielezea vipaumbele hivyo amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023, Shirika limeandaa vipaumbele kwa kuzingatia Mpango mkakati wa Shirika wa mwaka 2021/2022- 2025/2026.

Aidha ameeleza kuwa Shirika limetenga kiasi cha Sh. 2.7 Billioni kwa ajili ya kuimarisha ofisi saba za kanda ambazo ni Arusha, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam, Dodoma, Kigoma na Mbeya, kwa kuongeza wafanyakazi na vitendea kazi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakati na kuimarisha zoezi la ukaguzi wa mara kwa mara sokoni ili kupunguza bidhaa hafifu sokoni na hatimaye kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora na salama.

Ameeleza kuwa Shirika limetenga Sh. 1.6 Billioni kwa ajili ya kuandaa viwango 630 vya kitaifa katika sekta mbalimbali ili kuwezesha biashara kwa kumpa mzalishaji uhakika wa kupata masoko ya ndani na nje na kumhakikishia mlaji wa mwisho usalama na ubora wa bidhaa atakayotumia ikiwa ni pamoja na kuweka ushindani sawia wa bidhaa katika soko.

Ameongeza kuwa Shirika limetenga Sh. 261 Millioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za usajili wa bidhaa na majengo ya chakula na vipodozi ili kuhakikisha wananchi wanatumia bidhaa zilizo bora na salama.

Pia Shirika limetenga Sh. 581 Millioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uthibitishaji wa mifumo ya kiutendaji ambapo kwa sasa TBS imepatiwa ithibati ya kufanya shughuli hiyo na mashirika yanayoweza kuthibitishiwa ubora wa mifumo yao ya kiutendaji kupitia TBS. Mifumo hiyo itasaidia kuhakikisha wananchi wanapokea huduma zilizo bora.

Aidha Shirika limetenga Shilingi billioni 1.6 kwa ajili ya kuandaa viwango 630 vya kitaifa katika sekta mbalimbali ili kuwezesha biashara kwa kumpa uhakika mzalishaji wa kupata masoko ya ndani na nje. Pia, kumhakikishia mlaji wa mwisho usalama na ubora wa bidhaa atakayotumia ikiwa ni pamoja na kuweka ushindani sawia wa bidhaa katika soko.

Ameeleza kuwa Shirika limetenga Shilingi millioni 261 kwa ajili ya kuimarisha shughuli za usajili wa bidhaa na majengo ya chakula na vipodozi ili kuhakikisha wananchi wanatumia bidhaa zilizo bora na salama.

Aidha, Dk Ngenya amesema mashirika yanaweza kuthibitishiwa ubora wa mifumo yao ya kiutendaji kupitia TBS. Hii itasaidia kuhakikisha wananchi wanapokea huduma zilizo bora.

Shirika limetenga Shilingi milioni 800 kwa ajili ya kufanya shughuli za kuhakiki ubora wa vipimo ili kuhakikisha usahihi wa majibu ya vipimo mbalimbali kutokea maabara, mahospitalini na viwandani na kupelekea watoa huduma au maamuzi kufanya maamuzi sahihi" 

Ngenya

 

 

Post a Comment

0 Comments