JESHI LA ZIMAMOTO LIMEFANYA MABADILIKO YA TOZO DHIDI YA MAJANGA YA MOTO.

 ðŸ“ŒSALMA HAROUN

JESHI la Zimamoto na Ukoaji limefanya mabadiliko ya tozo za ukaguzi wa usalama dhidi ya majanga ya moto katika majengo na maeneo mbalimbali pamoja na utaratibu wa ukusanyaji tozo ili kuleta tija na kuliwezesha Jeshi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Awali Jeshi lilibeba jukumu la kumfata mteja na kuomba kufanya ukaguzi katika jengo, eneo au chombo cha usafiri ambapo kwa sasa umeonekana kuboreshwa zaidi.

Hayo yamesemwa Leo jijini Dodoma na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto, Puyo Nzalayamisi na kuwataka wateja au wamiliki wa majengo, eneo au chombo cha usafiri ambaye hajafanyiwa ukaguzi kufika ofisi za jeshi na kuomba kukaguliwa wakati bado wakiendelea kuboresha mifumo yao ili wateja waweze kuomba kupitia mitandao.

Amesema baadhi ya tozo zimefutwa kama vile mashamba ya kahawa, mikonge pamoja na chai lakini pamoja na kushuka kwa gharama hizo bado kuna maingizo mapya ya tozo ikiwa ni sehemu ya karakana, vituo vya usafirishaji na wafanyabiashara ya kufua nguo 'dry cleaner'.

Tunaendelea kuwasihi wamiliki wa majengo, maeneo pamoja na vyombo vya usafiri kufuatilia taarifa zetu kupata elimu, Sheria na nyaraka zingine kupitia mitandao yetu ya kijamii (Instagram @tanzimamoto, Twitter @tanzimamoto, Facebook @ Jeshi la zimamoto na ukoaji) na kuendelea kuwasiliana nasi kupitia namba zilizoainishwa kwa changamoto zote kuhusu mabadiliko haya

Aidha ameendelea kuwakumbusha wananchi kushiriki katika zoezi la sensa litakayofanyika Agosti 23 mwaka huu kwa maendeleo ya taifa kutokana na kuwasaidia katika zoezi la upangaji wa vitendea kazi pamoja na upangaji wa rasilimali watu katika vituo vyao vya kazi.

 

Post a Comment

0 Comments