MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA KATI YAANZA KWA KISHINDO.

 

📌RHODA SIMBA

TOFAUTI na Maonesho ya 88 ya mwaka jana, mwaka huu yameanza kwa mwamko zaidi kwa taasisi, kampuni na idara mbalimbali kuonesha bidhaa na zana za kisasa zaidi kwa ajili ya kuboresha na kuinua kilimo na ufugaji wenye tija zaidi.

CPC Blog imepita katika mabanda mbalimbali ya taasisi na kampuni mbalimbali zinazoonesha zana bora za kisasa kilimo na ufugaji na kuzungumza na waoneshaji ambao wameleta zana hizo ili kuhamasisha wakulima na wafugaji kuzitumia katika uzalishaji badala ya kutumia zana duni.

Akizungumza na mtandao huu Meneja wa Taasisi ya Kilimo (Agricom) Kanda ya Kati, Peter Temu alisema wamejiandaa kuonesha bidhaa lengo ni kuhakikisha wakulima na wafugaji wanapata zana za kisasa kuanzia uzalishaji shambani hadi sokoni.

Tofauti na maonesho ya mwaka jana ambayo walileta zana chache sababu ya Covid-19, Temu alisema, mwaka huu wameleta zana nyingi za kisasa za uzalishaji mazao kuanzia shambani hadi kuuza kwenye masoko mbalimbali

Temu amesema, wameletea katika maonesho hayo zana ambazo zinaleta na zinakusudia kuleta suluhisho kwa wakulima kuachana na kilimo cha kutomia jembe la mkono na kuanza kutumia zana za kisasa zinazouzwa kwa bei nafuu.

Mwaka 2021 tulileta zana chache, lakini mwaka huu, wameleta zana zote zinazotakiwa katika mnyororo mzima wa mazao bora tangu kwenye uzalishaji shambani hadi sokoni. Watatumia trekta tangu kulima, kupanda kwa kutumia planta, kupalilia na kuvuna kwa mashine

Wamewaletea wakulima matrekta, mashine ya kupiga haro, mashine za kupalilia na kuvuna ambazo zitauzwa kwa bei ya punguzo kwa mwezi mzima wa Agosti wakiwepo kwenye maonyesho.

Zipo mashine nyingi za kutosha ambazo zinaweza kulima, kupalilia na kuvuna dengu, mtama na mazao mengine na zinasaidia kupunguza muda kwa wakulima kutumia mikono.

Hata maonesho ya 88 yakiisha wana zana za kutosha zimeletwa na hivyo wataendelea kutoa huduma za kuuza zana za kisasa katika matawi zaidi ya 12 yaliyopo nchini.

Taasisi hiyo inajiita One Stop Solution kwa sababu ipo kwa ajili ya kuhakikisha wakulima wanapata zana zote ambazo zinatakiwa kuanzia kuandaa shamba hadi kuvuna shambani tofauti na zamani ambapo wakulima walitakiwa kutumia jembe la mkono,

Hivi sasa Agrocom imewaletea zana zote kwa ajili ya kuwafanya watabasamu kutoka shambani hadi sokoni.

Akizungumza Katibu Tawala Msaidizi (uchumi na Uzalishaji) Aziza Mumba amesema maandalizi yanaendelea kwa taasisi mbalimbali kujipanga kuonesha bidhaa katika mabanda yao.

Pamoja na taasisi za kilimo, zinazoonesha zana za kilimo, zipo taasisi zinazoonesha bidhaa za mifugo pamoja na taasisi za elimu ya juu, afya, ujenzi na bidhaa nyingine.

 

Post a Comment

0 Comments