MAPOKEO YA WANANCHI KUHUSU MAPUMZIKO YA SIKU YA SENSA AGOSTI 23/2022.

📌SALMA HAROUN & JOSEPHINE MTWEVE

KUFUATIA kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuridhia siku ya sensa kuwa ya mapumziko baadhi ya wafanyabiashara wa Jiji la Dodoma wametoa maoni yao ni kwa kiasi gani wataweza kuathirika na mapumziko hayo.

Akizungumza leo Shabani Ally ambaye ni mfanyabiashara wa nyama katika Soko kuu Majengo amesema kuwa utaratibu huo umekua wa tofauti ukilinganisha na sensa zilizopita ambazo zilikua zikiruhusu watu kwenda kufanya biashara zao.

Ally amesema kutokana na biashara anayoifanya kuna changamoto ambayo ataweza kuipata kutokana na kutofanya kazi siku hiyo hususani kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara za mali kuoza.

Kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza wateja kwasababu tuna wateja wanaokuja siku kadhaa katika wiki hivyo kwa wateja waliozoea kuja katika siku ya jumanne ambayo imegongana na siku ya sensa tutawapoteza

Kwa upande wake Willison Mazinga ambaye anajishughulisha na shughuli za ujenzi amesema kuwa itaweza kumwathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi yake anayoifanya ni ya kulipwa kila siku.

Aidha ameongeza kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya sensa ya watu na makazi hali ya kuwa yamebaki masaa machache kufikia zoezi hilo lakini kuna baadhi ya watu bado hawajaelimika.

Taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ilieleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia siku ya Jumanne Agosti 23 kuwa ya mapumziko na watu wote wanatakiwa kubaki nyumbani kwaajili ya kuhesabiwa.

Post a Comment

0 Comments