MH.ROSEMARY SENYAMULE AMEAHIDI KUENDELEZA ALIPOISHIA MTAKA

 

📌JOSEPHINE MTWEVE & SALMA HAROUN

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule ameahidi kuendeleza jitihada zilizofanywa na aliyekua mkuu wa mkoa huo Mh.Antony Mtaka mara baada ya kukabidhiwa ofisi katika kutekeleza majukumu ya kiserikali.

Hayo ameyasema leo Jijini Dodoma ambapo ameahidi kuendeleza ujenzi wa soko la machinga ambalo litajumuisha wajasiriamali wa mkoa huo kwa lengo la kufanya biashara na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha amewaomba viongozi wote wa Mkoa wa Dodoma kuyajua majukumu yao na kuyatekeleza ili kuweza kukamilisha yale yote yaliyoanzishwa na aliyekua Mkuu wa Mkoa huo Mh. Mtaka ili kuleta taswira nzuri katika Jiji la Dodoma.

Niombe ushirikiano wenu sana ili Dodoma hii inayotegemewa na watanzania iweze kuwa na sura inayotarajiwa

Kwa upande wake aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Antony Mtaka amemwomba aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa huo kuwapa vipaumbele vijana katika suala zima la fursa mbalimbali za kiofisi.

                                      

Amesema vijana wengi waliokua wamekosa ajira baada ya kumaliza masomo yao walijitolee kufanya kazi bila malipo ili kuweza kupata uzoefu kwa lengo la kutengeneza mazingira ya kupata kazi kwa urahisi.

Pia Mh. Mtaka amewashukuru wale wote ambao ameshirikiana nao katika kipindi chote cha majukumu yake mkoani Dodoma hususani waandishi wa habari kwa kufanya kazi pamoja kwa lengo la kuhabarisha jamii.

Mh Rosemary Senyamule anachukua nafasi ya Mh Antony Mtaka ambaye ameteuliwa kuma Mkuu wa Mkoa wa Njombe

 


 

Post a Comment

0 Comments