NDOTO ZA MAGRETH MAGABILA ZILIVYOKATISHWA KWA AJALI YA GARI.

 ðŸ“ŒAGNESS PETER, SALMA HAROUN & JOSEPHINE MTWEVE

KATIKA jamii kumekuwa na asilimia kubwa ya watu wanaopitia ugumu wa maisha na kuishi katika mazingira hatarishi kutokana na sababu tofauti za kimaisha na kupelekea kupotea kwa malengo na ndoto walizozitarajia katika kufanikisha hilo.

Magreth Magabila ni mwanamke aliyekuwa na ndoto za kuwa mama bora lakini mwenye kujishughulisha kama watu wengine lakini ndoto hizo zilipotea mara baada ya kupata ajali ya gari mwaka 2002 akitokea chuoni katika kijiji cha Homboro Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa mahojiano amesema ajali ilisababisha kuumia kwa kiasi kikubwa upande wa kichwani jambo lililomlazimu kufanyiwa upasuaji ili kunusuru maisha yake.

Sikuweza kupata malezi mazuri kutokana na kwamba nina mzazi mmoja ambae ni baba na mama ambae ni mama mdogo kwa hiyo hakulichukulia jambo la kidonda changu kichwani kwà uzito nikaanza kupata manyanyaso na kuambiwa nifanye kazi kama mtu ambae sijawahi kupata tatizo la aina yoyote

Licha ya Magreth kuwa na tatizo la kichwa, aliporuhusiwa kurudi nyumbani na kupewa masharti ya kulelewa kama mtoto mchanga lakini amesema alipata mateso makali alipokuwa akiishi na wazazi wake jambo lililopolekea kutohimili hilo na kutoroka nyumbani kwao.

Amesema baada ya kutoroka alikutana na msamalia aliyetaka kumsaidia kumsomesha lakini alipogundua ametoroka nyumbani alimshauri kurudi nyumbani kuomba msamaha kwà wazazi wake kisha akampa nauli ya kumsafirisha.

Magreth amesema kutokana na mama yake mdogo kuonekana kutopendezwa naye aliamua kuondoka na kuolewa ambapo mwaka 2010 mwezi wa 9 mumewe alivamiwa na kujeruhiwa vibaya katika biashara yake.

Mume wangu hakuugua sana alifariki mwezi huo huo na mateso yakaendelea kutokana na ndugu wa mume wangu kuninyang'anya hata vidogo nilivyokuwa navyo sikupata msaada wowote nikaanza kuhangaika

Kuanzia mwaka 2014 Magreth amesema alipata tatizo jingine la uti wa mgongo ambapo mwaka 2018 alishindwa kabisa kutembea na mnamo tarehe 23 mwezi wa Februari mwaka huu alipata msaada wa fedha za hospitali ambapo aligundulika kuwa pingili za uti wa mgongo zimepinda. 

Mpaka sasa Magreth anaishi Dodoma kwa kutegemea msaada wa wasamaria wema pamoja na watoto wake wawili wa kiume ambao ni wadogo kiumri na bado anahitaji msaada wa fedha za matibabu ili aweze kujishughulisha na kuwajibika kama watu wengine.

Post a Comment

0 Comments