OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA MWENENDO WA WATALII WALIOINGIA NCHINI JANUARY HADI JULAI 2022

 ðŸ“ŒAGNESS PETER

OFISI ya Taifa ya Takwimu imetoa rai kwa taasisi zinazotoa huduma kwa watalii kuendelea kuboresha zaidi huduma zao kutokana na umuhimu wa sekta ya utalii katika kuingiza fedha za kigeni kwa lengo la kuwavutia watalii ambao walishawahi kufika nchini.

Hayo yamesemwa Leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Daniel Masolwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema sekta ya utalii inachangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 17 na kuchangia mapato katika fedha za kigeni kwa takribani asilimia 25.

Amesema idadi ya watalii kutoka nje ya nchi waliotembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika kipindi cha Januari hadi Julai mwaka huu waliendelea kuongezeka hadi kufikia 742,133 ikilinganishwa na watalii 456,266 walioingia nchini mwaka 2021 ikiwa ni sawa na asilimia 62.7.

Watalii walioingia nchini mwezi Julai 2022 pekee waliongezeka hadi 166,736 ikilinganishwa na watalii 81,307 walioingia nchini mwezi Julai 2021 sawa na ongezeko la asilimia 105.1 na idadi ya watalii walioongezeka mwezi Julai 2022 ilikuwa zaidi ya mara mbili ya watalii walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2021

Aidha amesema idadi kubwa ya watalii walioingia nchini kutoka nchi zilizo nje ya bara la Africa kwa mchanganuo wa utaifa kwa kipindi cha Januari hadi Julai 2022 walitoka Marekani ikiwa na watalii 51,301.

Amesema nchini watalii kutoka bara la Africa ambapo katika kipindi Cha Januari hadi Julai walipokelewa kutoka Kenya kwa idadi ya watu 86,220, Burundi 54,877, Malawi 27,079, Uganda 21,080 na Afrika kusini 20,868.

Katika kipindi cha mwezi Julai pekee mwaka huu idadi kubwa ya watalii walioingia nchini walitoka Kenya 16,654, Burundi 7,966, Malawi 5,113, Afrika kusini 4,335 na Rwanda 4,035

Kwa mujibu wa Sera ya Mapitio ya Ofisi ya Takwimu, idadi ya watalii wanaoingia nchini zinaweza kufanyiwa mapitio endapo Takwimu mpya na zilizohusishwa kutoka kwenye chanzo zinapatikana.

Post a Comment

0 Comments