SERIKALI YAOMBWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA.

 ðŸ“ŒAGNESS PETER

KUFUATIA Jiji la Dodoma kuendelea kukua baadhi ya wananchi wa jiji hilo wameiomba Serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za maisha na kutoa elimu juu ya kutumia fursa zilizopo kutokana na wengi wao kushindwa kunufaika nazo.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma na baadhi ya wananchi ambapo Willson Masinga ambaye anajishughulisha na shughuli za ujenzi amewataka vijana kuwa na fikra za haraka katika kutambua nini kifanyike ili kuepukana na hali ngumu ya maisha.

Masinga amesema kutokana na maisha kuwa magumu imepelekea watu wengi kushindwa kuweka akiba kwasababu fedha nyingi zinatumika kupata mahitaji ya siku bila kubaki na akiba

Kwasasa vitu vimepanda bei sana kiasi cha pesa tunazopata zinatosha tu kununua mahitaji ya nyumbani hasa kwa sisi tunaofanya kazi za kujenga tunashindwa hata kuweka akiba ya pesa angalau tatizo likitokea zitusaidie au tu akiba ya kuanzisha biashara

Aidha Queen Samson ambae ni mfanyabiashara wa vifaa vya urembo ameiomba Serikali kupitia ngazi za mitaa kutoa elimu ya namna ya kujiajiri kupitia fursa ya muingiliano wa watu katika jiji hilo.

Amesema wingi wa watu ni fursa mojawapo ya kujiajiri kwa kufanya biashara ambazo si lazima Serikali itoe au iseme.

Hata hivyo amesema wapo baadhi ambao ni ngumu kupata mawazo ya haraka kuhusu nini kifanyike ili kutengeneza biashara kulingana na watu wa eneo husika hivyo Serikali ina wajibu wa kusaidia kutoa elimu.

Watu wengi huwa wanasubiri Serikali iseme au itoe fursa fulani ndio watu wachangamkie lakini sisi wenyewe tunawajibu wa kufikiria kujiajiri wenyewe na kuwa wabunifu kwasababu fursa zinapatikana kwenye wingi wa watu japo hata Serikali inawajibu pia wakutoa elimu

Kwa upande wake Hawa Sadock ameiomba Serikali kupunguza gharama za maisha ili kupata urahisi wa kujiajiri na kuweka akiba pamoja na kukuza jiji hilo kupitia shughuli za kiuchumi endapo bidhaa zitashuka bei.



Post a Comment

0 Comments