SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAUNGA MKONO SERA UWEKEZAJI NCHINI.

 

📌SALMA HAROUN

MENEJA wa Habari na uhusiano kupitia Shirika la nyumba la Taifa Muungano Kasibi Saguya ameeleza mpango unaounga mkono sera ya Mh Rais ya kuvutia uwekezaji nchini unaotarajiwa kuzinduliwa Septemba 2022.

Hayo yamwesemwa leo jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari, ambapo Meneja huyo amesema wataweza kuanzisha miradi mengine ya ujenzi wa majengo ya biashara katika maeneo mbalimbali nchi.

Aidha ameongoza kuwa wanaendeleza miradi ya ukandarasi ikiwemo ujenzi wa majengo ya ofisi za Wizara nane (8) jijini Dodoma.

Aidha Saguya amesema shirika linadai wadaiwa sugu kiasi cha shilingi Bilion 26 ambapo kati ya hizo billion 6 zitafutwa kutokana na baadhi ya wadaiwa kufariki,na makampuni mengine kutokuendelea kufanya kazi.

Tunatoa wito kwa wapangaji na wadaiwa sugu wa kodi ya pango kuhakikisha wanalipa kodi na malambikizo wanayodaiwa kwa kuwa shirika kuanzia sasa linajiandaa kukusanya kodi hii kwa asilimia 100

Amesema wanaendelea kutekeleza mpango maalum wa miaka mitano wa ukarabati wa nyumba za shirika utakaoisha mwaka 2027, kukarabati nyumba katika mikoa ya Dar -es salaam, Iringa, Tabora, Arusha, Kigoma, Morogoro, Lindi, Tanga, Mbeya, Mwanza, Singida na Kagera kwa gharama ya shilingi bilion Nane (8).

Shirika la Nyumba la Taifa lilianzishwa mwaka 1962 kwa sheria Na.45 likiwa na jukumu la kuwezesha ujenzi wa nyumba na majengo mengine kwa matumizi mbalimbali hususani makazi, Ofisi na biashara kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Shirika wa Miaka 10.

 

Post a Comment

0 Comments