SIDO YATOA MSUKUMO KWA VIJANA KUJIENDELEZA KIUCHUMI.

 ðŸ“ŒAGNESS PETER & SALMA HAROUN

SHIRIKA la huduma ya viwanda vidogo (SIDO) imetoa msukumo kwa wajasiriamali wanaojiwekeza katika maeneo ya kuzalisha mitambo na vitendea kazi mbalimbali kutumia fursa ya kupata elimu kupitia taasisi hiyo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi

Taasisi ya SIDO imejiratibu katika kutimiza wajibu wa kuanzisha na kuendeleza viwanda katika sekta ya teknolojia kwaajili ya kuhakikisha wajasiriamali wanapata mahitaji stahiki yanayohitajika

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mratibu wa miradi (SIDO), Stephano Martini Ndunguru ambapo amewataka vijana kuambatana na taasisi hiyo katika kupata mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kuwafungua kimtazamo katika kuhakikisha wanaweza kujihimili.

Aidha amesema baada ya kumaliza mafunzo kwa wanaoshughulika na mazao au bidhaa zinazohitaji kuthibitishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) watawaunganisha nao ili kujiridhisha kuwa bidhaa zao zimekidhi viwango vya ubora kwa matumizi sahihi.

Tunakuwa na eneo la mafunzo ya ujasiriamali na huduma za ugani na ni kwa nadharia na vitendo ambayo inalenga moja kwa moja kumfungua mjasiriamali au mtanzania yoyote katika mtazamo ili aweze kuhimili katika kuhakikisha mazingira yake yanamungiza kipato

Kwa upande wake Halphan Amini ambae ni fundi wa kuchomelea katika taasisi ya SIDO amewashauri vijana kutumia fursa za taasisi hiyo katika kupambana kufanya kazi ili kujikimu kiuchumi

Naye Majaliwa Samweli aliyejiajiri mwenyewe amewataka vijana kusimama na kujitambua kwa kujiajiri wenyewe kwa kutokutegemea serikali iwaajiri.

Ukionyesha kitu hata serikali inaweza kukutazama na kuweza kukusaidia lakini ukibaki mtaani na kubweteka hata watu watakutelekeza


 

Post a Comment

0 Comments