TIC YATOA WITO KWA UMMA KUFANYA UWEKEZAJI KUPITIA FURSA MBALIMBALI NCHINI

 ðŸ“ŒAGNESS PETER

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya kati Dodoma kinatoa wito kwa vijana kufanya uwekezaji kupitia fursa mbalimbali pamoja na kutoa elimu kupitia warsha na semina kwa wajasiliamali wadogo, wakati na wakubwa kwa lengo la kuwajenga kitaalamu.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Kaimu Meneja wa Kituo cha uwekezaji Kanda ya kati Juma Ally Nzima ambapo amesema kupitia kituo hicho vijana wamenufaika kwa kuwezeshwa kutazitambua fursa mbalimbali zilizopo ambazo zina manufaa ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo.

Nzima amesema kupitia taasisi mbalimbali wanatoa elimu kwa umma hasa vijana ili kuwapa uwezo wa kupata taarifa tofauti na kufanya zana nzima za uwekezaji.

Kwa muktadha wa TIC uwekezaji ni shughuli ya kiuchumi ambayo lengo lake ni kuwekeza fedha kwaajili ya kupata faida na kutengeneza ajira na kuinua uchumi wa nchi kwa mawanda mapana

Aidha amesema moja ya jukumu la kituo hicho ni kuishauri serikali kuhusu Sera rafiki za uwekezaji nchini kwa lengo la kukuza uwekezaji nchini.

Kwa upande wake Emmanuel Paulo ambae ni mkazi wa Jiji la Dodoma ameomba serikali kuangalia namna ya kuwawezesha vijana kupata kipato cha uwekezaji kutokana na changamoto za vipato hasa kwa wale wanaotoka vyuoni.

Amesema muitikio kwa vijana katika uwekezaji ni mdogo kutokana na uhaba wa elimu ya kutosha juu ya suala hilo hivyo taasisi husika ziongeze nguvu ya kutosha katika utoaji mafunzo.

Jenipha Antony mkazi wa Jiji la Dodoma ameiomba serikali kutoa ajira kwa wingi ili kupunguza ongezeko la vijana wasio na ajira mtaani kwa lengo la kuwapa uwezo wa kujiwekeza katika sekta mbalimbali pamoja na kupata mikopo ya kuanzisha biashara.

Nipende kuishauri taasisi ya TIC waweze kufanya jitihada za kuwafikia vijana popote pale wanapokuwa wanapatikana iwe mjini au ndani vijijini watu wanashindwa kufikiwa na kupewa elimu kwahiyo kama wataweza kuwafikia hawa vijana itakuwa fursa kubwa kwao

TIC ni taasisi ya Umma yenye jukumu la kuhamasisha, kuhimiza, kufanikisha, kuratibu masuala ya uwekezaji pamoja na kufanya shughuli mbalimbali za kutangaza fursa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kukuza uwekezaji Tanzania.  

Post a Comment

0 Comments