TUME YA TEHAMA IMESEMA MPAKA KUFIKIA MWAKA 2025 ITACHANGIA ASILIMIA 3 YA PATO LA TAIFA

 

📌RHODA SIMBA

TUME ya TEHAMA nchini imesema imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba inachangia asilimia tatu (3%) ya pato la taifa ifikapo mwaka 2025.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Dkt. Nkundwe Mwasaga jijini Dodoma wakati akielezea shughuli mbalimbali za tume hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 ambapo ametaja mikakati hiyo ni kuhakikisha wanakuwa na uwekezaji mkubwa katika TEHAMA na kuwa kivutio kwa makampuni makubwa Duniani ya masuala ya TEHAMA kuja kuwekeza nchini.

Dkt. Nkundwe amesema kuwa katika kutekeleza mikakati hiyo tume hiyo imepewa majukumu ya kuhakikisha inakuza na kuendeleza wataalamu wa sekta ya TEHAMA, inakuza na kuendeleza makapuni madogomadogo ambayo yameshikilia ajira nyingi za watanzania pamoja na kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha uchumi wa kidigiti.

Hii tume tumepewa majukumu makubwa tu ila bado tutanatakiwa kuhakikisha tunakuwa na uwekezaji mkubwa katika TEHAMA na kuwa kivutio kwa makampuni makubwa Duniani ya masuala ya TEHAMA kuja kuwekeza nchini kwetu kwa maana hiyo ni lazima tufanye kazi kwa kila namna ili sekta hii iwe kitovu cha uchumi wa Taifa hili

Dkt.Nkundwe

Na kuongeza kuwa 

Tanzania kwa sasa inategemewa kwa kiasi kikubwa sana na nchi za jirani kwa upande wa mitandao na hili ni jibu tosha kuwa Sekta ya TEHAMA inafanya vizuri na tutaendelea kufanya vizuri

Dkt.Nkundwe

Dkt.Nkundwe amebainisha kuwa sekta ya TEHAMA itakuwa kitovu cha uchumi wa taifa endepo kila mmoja akitumia mtandao kwa faida na sio kwa matumizi mabaya.

Hata hivyo Dkt.Nkundwe ameongeza kùwa sekta ya TEHAMA kwa sasa inakuwa kwa kasi hasa kwa biashara za mtandaoni ambapo watanzania kwa sasa wanaweza kupata huduma hata wakiwa majumbani mwao na hiyo pekee inatosha kusema kuwa matumizi ya mtandao yameleta mapinduzi ya kiuchumi kwa sasa badala ya kutumia pesa na muda mwingi kuzunguka kutafuta bidhaa unatumia tu mtandao na unapata huduma.

Biashara mtandaoni kwa sasa imekuwa kwa kasi sana hapa nchini na imesaidia kuokoa fedha na muda kwa wananchi kwani hata ukiwa nyumbani kwako huna haja ya kusafiri unaingia tu mtandaoni unaagiza bidhaa inakufikia popote ulipo hiyo ni moja ya faida za sekta ya TEHAMA 

Dkt.Nkundwe

Ameongeza kuwa kwa vipimo vya dunia Tanzania inashika namba moja kwa kuwa na watu wengi wanaotumia huduma za kibenki mtandaoni kwani teknolojia hiyo imewavutia wengi kwa sababu inawasaidia kuokoa muda na pesa wakati wa kufuata huduma hiyo kwenye matawi ya benki.

Pia Dkt.Nkundwe amezungumzia zoezi la uwekaji wa Anwani za Makazi kuwa itakuwa miundombinu muhimu sana kwa sekta ya TEHAMA hivyo akatoa rai kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja anaingia katika mfumo huo wa postikodi.

Anuani za makazi zinatusaidia sana sisi wa sekta ya TEHAMA kufanya kazi zetu kwa urahisi na kwa muda mfupi pia maana imekuwa rahisi sasa kufika eneo flani kwa mtu husika kupitia data zilizopo katika mfumo wa anuani yake kulingana na eneo alilopo

 Dkt Nkundwe.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa ameipongeza tume hiyo na kusema kuwa Tanzania sasa ipo ndani ya nchi kumi bora duniani kwa kuwa na gharama za chini za mitandao hivyo ni lazima kuona kazi kubwa inayofanywa na serikali kupitia tume hiyo ya TEHAMA.

Kuna nchi ukifika kununua tu bando la GB 1 sio chini ya dola za kimarekani mia nne sasa fikiria hiyo pesa ukiibadisha kwa fedha zetu hapa itakuwa shilingi ngapi, ndio maana nawambia sisi bado tupo chini sana katika kupata huduma hizi za mtandaoni

Msigwa



 

Post a Comment

0 Comments