WANAWAKE ILAZO WATAKIWA KUTENGENEZA VIKUNDI KWAAJILI YA KUPATA MIKOPO INAYOTOLEWA NA SERIKALI


📌AGNESS PETER

WANAWAKE wa mtaa wa Ilazo Jijini Dodoma wametakiwa kuunda vikundi vya watu watano na kujisajili katika ofisi ya serikali ya mtaa huo ili kupata mikopo iliyotolewa na Serikali kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa mtaa wa Ilazo Moses Mazengo, leo Jijini Dodoma ambapo amewataka wanawake kujitokeza na kutumia fursa hiyo ya kupata mikopo ili iwasaidie katika kukidhi mahitaji yao.

Moses amesema Serikali inatoa mikopo isoyokuwa na riba lakini bado muitikio ni mdogo kutokana na masharti yaliyowekwa wakati wa kuchukua fedha hizo.

Imekuwa changamoto kwa akina mama kutokana na masharti yaliyopo, wanashindwa kujisajili ili Serikali iwatambue maana hata fedha zinapotoka zinatakiwa kujulikana zinaenda kwa akina nani. Serikali inataka kutambua kama mtu anataka mkopo, ana malengo gani au vyanzo vya biashara yoyote? ndio sababu usajili unatakiwa.

Amesema serikali inashauri viundwe vikundi na vianze kujiendesha kabla ya kuchukua mkopo ili kutengeneza vyanzo vya biashara na si kusubiri fedha ya Serikali ndiyo ianzishe mtaji.

Kwa upande wake Lilie Samson ambaye ni mkazi wa eneo hilo amesema kutokana na mikakati ya kupata mikopo hiyo ni mrefu hivyo inapelekea wengi wao kushindwa kujisajili.

Amesema ni rahisi kujiunga na vikundi vya akinamama vya mtaani kutokana na taratibu zake hazihitaji mambo mengi kama ilivyo kwa Serikali

Inatakiwa kuunda kikundi cha watu watano baada ya hapo tunatakiwa kumfata bibi maendeleo wa mtaa atoe maelekezo ya namna ya kujisajili kisha kuandika barua ambazo zinatakiwa kwenda manispaa na kusubiri fedha kutoka kwa Mwenyekiti baada ya kujulikana Serikalini.

Aidha Christopher Peter mkazi wa eneo hilo, amesema akinamama wanashindwa kujiunga na vikundi kupata mikopo ya serikali kutokana na kushindwa kutengeneza malengo ya fedha hizo na kutokuwa na vyanzo vya biashara ya kuzalisha fedha.

 

Post a Comment

0 Comments