WAZIRI MASHIMBA AZITAKA TAASISI ZINAZOFANYA TAFITI ZA MBEGU NA MIFUGO ZIWAFIKIE WANANCHI.

 

📌RHODA SIMBA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amezishauri Taasisi zinazofanya utafiti wa mbegu za mifugo na mazao kuhakikisha tafiti hizo wanazofanya zinawafikia wananchi ili wanufaike nazo.

Waziri ametoa ushauri huo jijini Dodoma wakati akifungua maonesho ya nane nane kanda ya kati ambapo amesema tafiti nyingi zinazofanywa na watafiti haziwafikii wananchi kutokana na kushindwa kumudu gharama.

Amesema kuanzia mwaka 2023 hadi 2027 Serikali imepanga kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya mifugo kwa kuwaelimisha wafugaji kufuga kibiashara kwa kuwapatia elimu ya kuwa na mbegu bora za mifugo ya kisasa huku akisisitiza ubora wa bidhaa ni muhimu ili kushindanisha katika soko la ndani na nje ya nchi.

Kumekuwa na Taasisi nyingi ambazo zinahusika na kutoa elimu juu ya mbegu bora za ufugaji ambao unaweza kukuingizia kipato kikubwa

Na kikubwa zaidi mzingatie ubora wa bidhaa ambazo mnanunua na kuuza ili pia muweze kushindanisha katika masoko makubwa yaliyopo ndani na nje ya nchi 

Ameongezea kwa kuzitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanashirikiana na watoa huduma kuweka hereni mifugo yote mpaka ifikapo tarehe 30 Septemba mwaka huu zoezi hilo liwe limekamilika.

Zoezi hili ni muhimu sana linarahisisha kufuga mifugo kibiashara na inaongeza thamani ya mifugo yetu zoezi hili litapunguza unyang'anyi na wizi wa mifugo yetu kwahiyo naomba kuanzia Halmashauri zote za mikoa mzingatie hili suala mpaka ifikapo tarehe 30 Septemba muwe mmeshakamilisha zoezi hili la kuvalisha mifugo hereni

Ndaki

 Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema Dodoma ndio makao makuu ya Serikali hivyo wafugaji na wakulima wanaotakiwa kulima na kufuga kisasa licha ya Dodoma kuwa na machinjio ya kisasa bado kumekuwa na changamoto ya mifugo michache inayochinjwa katika machinjio hiyo ya kisasa iliyoko Kizota.

Tunalo eneo kubwa sana la kisasa na eneo hili linakadiriwa kuwa ni hekta milioni Moja (1) na Laki Mbili (2) ambayo ni kama 29% ya Mkoa mzima wa Dodoma, kwahiyo unaona eneo hili ni kubwa la kufugia

Na kwa Mkoa wa Dodoma tuna sifa zote za kufuga kwa maana ya eneo na kwa maana ya idadi ya kufuga na kazi tuliyokuwa nayo ni kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa

Senyamule

 Naye Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina amesema kutoka mwaka 2023 hadi 2027 Serikali imepanga kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya mifugo kwa kuwaelimisha wafugaji kufuga kibiashara kwa kuwapatia elimu ya kuwa na mbegu bora za Mifugo ya kisasa ili kumfanya mfugaji akue kisasa na kuwa na mifugo yenye tija.

 

Post a Comment

0 Comments