WIZARA YA KILIMO YATAKIWA KUFANYA KAZI NA SHIRIKA LA TAIFA LA BIMA

 

📌SALMA HAROUN

MAKAMU wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ameitaka Wizara ya Kilimo kufanya kazi na shirika la Taifa la Bima ili kuhakikisha wakulima hawapati athari zozote katika kilimo dhidi ya madhara yatokanayo na mbegu zisizo bora.

Hayo ameyasema leo Agosti 1 Jijini Mbeya katika maonyesho ya sikukuu ya Nanenane wakati akipita katika mabanda ya waliohudhuria maonyesho hayo. Mpango amesema suala hilo waweze kulifanyia kazi ili wakulima waepukane na changamoto katika kupata mbegu zisizo bora ambapo huwasababishia wakulima hasara wakati wa mavuno.

Amesema kuwa shirika la Utafiti la TARI katika kuwa wabunifu wanatakiwa kufanya utafiti kwenye mazao mbalimbali yatakayoweza kutumika katika maeneo tofauti kulingana na ardhi iliyopo nchini.

Kuna mbegu zimeenda kwa wakulima Wilaya ya Katavi zimeleta balaaa hazikuzaa wakulima wamesema TARI imetudanganya, turekebishe taasisi ya TARI ili kuleta ubora wa mbegu

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Mh Husseni Bashe, amesema ameziagiza Halmashauri zote kuwa wakulima waliotakiwa kulipia mbegu hizo wasilipie mwaka huu ili kuweza kuwapunguzia makali ya athari walizo zipata mwaka jana

Amesema wakulima wawe na utayari wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa ambapo pia ni chanzo kimojawapo cha mazao kutokubali katika maeneo yao.

Wakulima walifundishwa kupanda zao la alizeti wakati mvua zinaendelea kunyesha, wakati wakulima wamepanda hali ya hewa haikuweza kukubali na kupelekea wakulima kuathirika hususani katika nyanda za juu kisini.

 

 

Post a Comment

0 Comments