AMETT YAMTUNUKU NISHAI RAISI SAMIA.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

WAHANDISI na Mafundi Sanifu wa Vifaa Tiba Tanzania (AMETT) wamemtunuku nishai Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake katika kuboresha teknolojia ya afya nchini.

Akipokea nishai hiyo Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel alisema Rais Samia ameendelea kutambua sekta ya afya kama kiungo muhimu kwa taifa.

Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja ametoa ajira nyingi za wataalamu wa teknolojia ya vifaa tiba.

AMETT wamefurahishwa na mchango wa Rais Samia katika kuboresha teknolojia ya afya nchini kwa niaba ya Waziri wa Afya nimekuja kuchukua nishani ambayo wametoa kwa kutambua mchango wake.

Amesema kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kununua teknolojia ya vifaa tiba watoto wote wametibiwa ndani ya nchi.

Kutokana na uwekezaji huo serikali imeokoa zaidi ya sh.bilioni 17 ambazo zilikuwa zitumike kuwatibia watoto 500 nje ya nchi lakini sasa tunafurahi kutokana na uimara wa serikali yetu watoto hao wametibiwa nchini na serikali imeokoa fedha hizo

KUHUSU EBOLA

Kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebora Naibu Waziri aliwatoa hofu wananchi kuwa Tanzania iko salama na hakuna mgonjwa aliyegundulika hadi sasa.

Amesema serikali tayari imeanza kuchukua hatua za kujilinda ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila mtu anayetoka katika nchi zinazotuzunguka anapimwa kabla ya kuingia nchini.

Ni kweli jirani zetu ugonjwa wa ebora umeingia na kwasababu na sisi na wao tuna muingiliano tunafanya shughuli pamoja tunaendelea kuwaasa wananchi wetu kila mtu achukue hatua za kijilinda haraka. Maeneo yote ya mipakani tumetoa maagizo kwa waganga wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wizara kuhakikisha kila mtu anayeingia nchini kutoka nchi zote zinazotuzunguka anapimwa.

Upimaji huo utaenda katika viwanja vya ndege. Kikubwa tunachoweza kusema bado nchi yetu ni salama bado tunaendelea kuangalia mipaka yetu na hakuna mgonjwa hata mmoja.

Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pamoja na kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali na wataalamu wa afya.

 

Post a Comment

0 Comments