NIT YAJA NA MASHINE YA KUOSHA GARI KWA KUTUMIA DAKIKA 3

 ðŸ“ŒASHA MWAKYONDE

MBUNIFU na mwanafunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), katika kozi ya uhandishi wa Mitambo, Helen John amebuni mashine ya kuosha gari 'Automatic Car Washing Machine' ambayo ina hatua tano katika ufanyaji kazi wake wa kuosha hadi kukamilika ambapo inatumia dakika 3 na sekunde 49 hadi gari hilo kukamilika. 

Akizungumza leo Septemba 22,2022, kwenye maonesho ya maadhimisho ya Siku ya wahandisi Jijini hapa katika banda la NIT, Heleni amesema lengo la kubuni  mashine hiyo ni kutunza muda pamoja na kupunguza matumizi mengi ya maji huku akisema kwa sasa magari yamekuwa mengi mtu anapeleka gari kuosha anakaa zaidi ya saa mbili akisubiria foleni yake.

Amefafanua kuwa hatua hizo tano katika uoshaji gari ni kwamba kuna kifaa cha maji masafi, sabuni, brashi la kusafishia gari, maji ya kulisuuza na baadae kukausha hatua hizo zikikamilika gari hiyo itakuwa imeshatakata na kukaushwa.

Amesema mfumo huo unatunza muda zaidi na kwamba kwa siku mtu anaweza kuosha magari mengi zaidi ikilinganishwa na wale wanaoosha kwa kutumia mikono hivyo mashine hiyo inatumia dakika 3 na sekunde 49.

Kwa kawaida gari inaoshwa dakika 15 na zaidi lakini kwa kutumia mashine hii kwanza ina okoa muda pia mmiliki hatatumia nguvu kuosha gari kwani mashine ndiyo itafanya kazi sio mikono

Helen.

Helen ametoa wito kwa serikali kuziendeleza bunifu zao kwa kuwa dunia ya sasa ni ya sayansi na teknolojia hivyo suala la utunzaji muda ni la muhimu katika maendeleo.

Kwa upande wake Mkufunzi Uhandisi wa Matengenezo ya ndege kutoka NIT, Castory Njako amesema kuwa miongo mwa bunifu zilizofanya vizuri chuoni hapo na baadae zikashindanishwa wakati wa maonesho ya Siku ya wahandisi wanawake bunifu hizo zilishinda.

Aidha amewakaribisha wananchi wa Dodoma kwenda kuona fani za uhandisi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho huku akiwahamasisha vijana kujiunga.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments