TAMBO ZATAWALA KUELEKEA NMB,BUNGE BONANZA

 


📌RHODA SIMBA

BENKI ya NMB imeandaa bonanza la "kivumbi na jasho" ambapo timu za bunge na Benki za NMB zimetambiana katika bonanza kubwa la michezo leo huku kila upande ukieleza kujiandaa zaidi.

Bonanza hilo la ‘Kivumbi na Jasho’ litafanyika leo jumamosi katika viwanja vya Chinangali Park mjini Dodoma huku Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna alisema jana kuwa NMB ni moto wa kuotea mbali na imeandaa bonanza hilo mahsusi kwa wabungena NMB.

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa wabunge, Zaipuna alisema tofauti na miaka mingine lakini safari hii wameiandaa vema timu ya NMB na wako tayari kwa ushindi dhidi ya timu za wabunge.

Mtendaji huyo alisema wachezaji wote ndani ya timu hiyo watakuwa ni watumishi wa NMB kwa alichokieleza kuwa hakuna mamluki waliowaingiza na kuitambia timu ya wabunge kuwa NMB imejipanga kikamilifu.

Leo tunakabidhi vifaa hivi vya michezo vyenye thamani ya Sh20 milioni na kesho tutakabidhi vifaa vyenye thamani ya Sh50 milioni kwa ajili ya Hospitali ya Uhuru, lakini niwaambie bonanza hili la kivumbi na jasho haachwi mtu
Ruth Zaipuna.

Alitaja lengo la kucheza na wabunge ni kuendeleza mashirikiano waliyo nayo tangu siku nyingi kati yao na mhimili huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bunge Sports Club Abbas Tarimba alionya timu ya NMB kuacha kuingiza wachezaji wasio watumishi (mamluki) lakini akasema lazima bunge itashinda.

Tarimba alisema michezo na benki hiyo ni sehemu ya kuwaanda na kuwaimarisha wabunge kabla ya kwenda kwenye mashindano ya mabunge ya Afrika Mashariki.

Mbunge huyo wa Kinondoni alipongeza maandalizi waliyofanyiwa na NMB kwenye michezo ya mwaka jana kwamba yaliwaimarisha hata walipokwenda mashindano ya mabunge ya Afrika Mashariki, Tanzania ilichukua vikombe vyote kwa michezo nane.

Hata hivyo  amesisitiza kuhusu bonanza hilo kwamba wabunge wanalichukulia kama kipimo kwao hivyo wachezaji wa benki wajiandae kwa mashindano siyo mchezo wa bonanza.

 

Post a Comment

0 Comments