WIZARA YA AFYA YAANZA KUTOA ELIMU KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA.

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

WIZARA ya afya imeanza kutoa Elimu kwa jamiii na kutaka kuchukua hatua ili kukabili magonjwa yasiyoambukiza ambapo yamekuwa mzigo mzito kwa taifa.

Mkurugenzi wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Dk James Charles Kiologwe amewaambia waandishi kwa njia ya mtandao kuwa Serikali imeamua kutoa Elimu hiyo kwa kutumia waandishi wa habari katika mapambano hayo ili kuwafikia wananchi wengi kwa haraka na uhakika.

Ametaja takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2016 zinazoonyesha kuwa asilimia 71 sawa na vifo milioni 42 vilitokea Duniani kutokana na magonjwa hayo.

Asilimia 25 ya vifo hivyo vilihusu umri wa miaka 30 hadi 70

Dk Kiologwe 

Hata hivyo amesema magonjwa yasiyoambukiza ni mzigo kwa taifa na kwamba uzito kupita kiasi na unene kupindukia vinasababisha asilimia 73 ya magonjwa hayo.

Amesema vichocheo vingine ni changamoto za lishe zinazosababisha magonjwa hayo kwa asilimia 32 na matumizi ya tumbaku kwa asilimia 14.8

Dk Kiologwe aliongeza kuwa watu wanaofanya ngono isiyo salama kwa sasa ni wachache kuliko idadi ya watu kwenye uzito uliopitiliza viwango na kwamba mzigo unaongezeka zaidi huku theluthi mbili hawajitambui na kuchukua hatua .

Wengine wanafika hospital wakiwa na madhara ya kiafya zaidi 

Dk Kiologwe

Kwa mujibu wa tafiti zilizopo kwa miaka 10, visababishi vimeongozeka kwa magonjwa yasiyoambukiza kuliko magonjwa ya kuambukiza.

Vihatarishi vinavyosababishwa na lishe isiyo sahihi vinafikia asilimia 18 na vihatarishi vya matumizi ya pombe ni asilimia 15.9 alisema Dk Kiologwe na kuongeza tabia bwete, ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi ni vyanzo vikuu vya kupata magonjwa yasiyoambukiza

Dk Kiologwe

Ili kukabiliana na janga hilo Serikali imeamua kuunda timu kwa kila Mkoa ili kutoa Elimu ya magonjwa yasiyoambukiza na matarajio ni kushirikisha vyombo vya habari na kuandaa tuzo kwa waandishi wanaoandika habari zinazohusu magonjwa hayo.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments