CHUO CHA MIPANGO VIJIJINI CHATAJA VIPAUMBELE VYAKE KATIKA MWAKA WA FEDHA 2022/23

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

CHUO cha Maendeleo Vijijini kimeeleza vipaumbele vyake katika mwaka wa fedha 2022/23 kuwa kimeongeza udahili na usajili wa wanafunzi kutoka 14,417 mpaka kufikia wanafunzi 16,663 na kuendelea kufanya tafiti na kutoa huduma za ushauri na uelekezi kwa kufanya tafiti saba na kuandika kitabu kuhusu maendeleo vijijini.

Hayo yameelezwa leo tarehe 21 Oktoba 2022 na mkuu wa chuo hicho Prof Hozen Mayaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti katika chuo hicho katika mwaka wa fedha 2022/23.

Prof.Mayaya ameeleza kuwa chuo hicho kinaendelea kupitia mitaala ya mafunzo ya muda mrefu na kuandaa mitaala ya kozi mpya na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga miundombinu ya kufundishia.

Akiendelea kutaja vipaumbele ameeleza kuwa chuo kinaendelea kuajiri watumishi wapya, kulipa stahiki mbalimbali, kupandisha vyeo watumishi waliokidhi vigezo pamoja na kuboresha huduma za ustawi na kuongeza uwezo wa kielimu na kiutendaji kwa watumishi 396.

Aidha ameeleza kuwa chuo hicho kimejipanga kufanya ukarabati mkubwa na mdogo wa nyumba 13 za watumishi, kulipa madeni ya watumishi na watoa huduma, kutekeleza shughuli ambazo hazikutekelezwa katika Mpango Mkakati wa mwaka 2016/17-2020/21 pamoja na uendelezaji wa maeneo ya Miyuji Kaskazini, Chigongwe na Kiseke.

UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA CHUO KWA KIPINDI CHA MWAKA WA FEDHA 2021/22

Kuhusu utekelezaji wa majukumu ya chuo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 Prof Mayaya ameeleza kuwa hadi kufikia Juni 2022, jumla ya watumishi 351 walipata mafunzo ya muda mfupi na watumishi 50 wanaendelea na mafunzo ya muda mrefu ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwa Jumla ya Shilingi bilioni 9 zimetumika kugharamia utekelezaji wa miradi ya uendelezaji na utunzaji wa miundombinu ya chuo ambapo Shilingi bilioni 5 zimetumika katika ujenzi wa kumbi Tatu za mihadhara na mabweni mawili ya wanafunzi wa kike

Ameeleza kuwa kati ya Sh.bilioni 9, Shilingi bilioni 4 ambazo ni mapato ya ndani zimetumika kutekeleza miradi katika Kituo cha Mafunzo kilichopo Mwanza ikiwemo ujenzi wa mgahawa, jengo la utawala, maktaba na kununua ardhi kwa ajili ya upanuzi wa chuo.

Sambamba na hilo ameeleza kuwa katika mwaka wa masomo 2021/22, chuo kimeendesha program za muda mrefu 31.

Mpaka kufikia Juni 2022, washiriki 31 wa nje wamepatiwa mafunzo ya muda mfupi.

Kwa mwaka 2021/22, chuo kimesajili jumla ya wanafunzi 14,461. Aidha, jumla ya Wahitimu 8,200 wamehitimu mwezi Disemba, 2021 

Katika mwaka wa fedha 2021/22, chuo kiliwezesha wahadhiri wake kufanya tafiti Saba zinazolenga kutatua matatizo ya kijamii, kiuchumi na kuchangia kuandaa sera na miongozo mbalimbali ya kitaifa.

Chuo kinatekeleza mradi wa "Higher Education for Economic Transformation" ambao umetenga Shilingi bilioni 6.85 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia, kujifunzia kwa kujenga jengo moja la taaluma, kuboresha mitaala na kuwajengea uwezo Wahadhiri

Prof.Mayaya.



 

Post a Comment

0 Comments