HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA YAOKOA FEDHA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 4.43 KWA WAGONJWA AMBAO WANGETIBIWA NJE YA NCHI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

IMEELEZWA kuwa Hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) imefanikiwa kupandikiza figo kwa watu 31 na kuokoa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bil 2.3 huku ikitibu watu 715 ugonjwa wa moyo na kati yao 39 walibainika na matatizo ya moyo na kuwekewa vipandikizi na kati yao 8 wamepandikiziwa betri kwenye moyo.

Hayo yameelezwa  leo na Dkt. Alphonce Chandika Mkurugenzi Mtendaji wa (BMH) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya hospitali hiyo na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2022/ 2023

Amesema watoto 14 waliozaliwa na shida ya moyo wametibiwa huku watoto 10 wakifunguliwa vifua na kufanyiwa upasuaji.

Uwepo wa maabara hii ni uwekezaji muhimu wa kuokoa maisha ya wananchi hususani hapa makao makuu ya nchi kwahiyo tuna wananchi wawili ambao walihudumiwa kwa dharula na wakaokolewa maisha yao, kuna baadhi ya wagonjwa ambao mapigo yao huwa yanaenda taratibu na chini hivyo huwa tunawawekea betri ya kuongeza mapigo ya moyo na kupitia maabara hii huwa tumeweza kuhudumia watoto waliozaliwa na matatizo ya matundu ya moyo

Dkt Chandika

Aidha Dkt Alphonce amesema Bilioni 1.28 zimeokolewa kwa kuwafanyia upasuaji wagonjwa 58 wa nyonga kwa kuwawekea vipandikizi kwa gharama ya shilingi milioni 12 badala ya kutibiwa nje ya nchi kwa kiasi cha shilingi milioni 35 kwa mgonjwa mmoja.

Ukiangalia kwa hawa wagonjwa 56 tumeweza kuokoa jumla ya shilingi Bilioni 1.28 za kitanzania ambapo pesa hizo zilitakiwa zikawatibie hawa watu nje ya nchi 

Dkt Chandika 

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema BMH imeanza kutoa mafunzo kwa wataalamu wa usingizi na ganzi na tayari wataalamu 127 wamehitimu huku akibainisha kuwa Hospiltal hiyo inakwenda kuongeza wigo wa huduma kwa kujenga jengo maalum kwaajili ya matibabu ya moyo, upasuaji wa mifupa na ubongo ili kuhakikisha hospital hiyo inakuwa ya pili ya taifa.

Tunatarajia hizi huduma pia tuweze kujenga jengo kubwa kwaajili ya huduma za ugonjwa wa moyo maana ndio yanakuja kwa kasi tunatarajia mpaka 2025 tuwe tumekamilika

 Dkt Chandika 

 

 

Post a Comment

0 Comments