📌RHODA SIMBA
MAKAMU
wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Mohamed
Abdullah amesema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa matokeo ya mwanzo ya
sensa ya watu na makazi yaliyofanyika tarehe 23 Agosti 2022 yamefikia
asilimia 85 ambapo mgeni rasmi wa hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rais Samia
Suluhu Hassan.
Akizungumza
Jijini Dodoma katika maandalizi ya hafla hiyo yatakayofanyika Oktoba 31
katika uwanja wa Jamhuri amesema kuwa sensa ya mwaka huu ni yakipekee
na ya kisasa Kwa sababu imefanyikia kidigitali.
Sensa ya mwaka huu ni ya kisasa na yakipekee sababu imefanyikia kidigitali kuliko sensa za awamu yote na takwimu hizi zitatusaidia katika maendeleo mbalimbali ya kiuchumi
Kadhalika
amesema kuwa sensa hiyo haitatumika Tanzania pekee bali itatumika kwa
nchi nyingi duniania kwakuwa tumekuwa tukishirikiana na Nchi mbalimbali
katika mambo tofauti tofauti.
Sambamba
na hayo amesema takwimu za matokeo ya sensa zitasaidia Kwa kiasi
kikubwa shughuli za kiuchumi na kijamii ili kupanga maendeleo kwa
maslahi ya Taifa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema
maandalizi ya yanaendelea vizuri ambapo wameunda kamati 11
zinazoongozwa na Wakuu wa Wilaya .
Amesema
kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na vyombo
vingine wamehakikisha suala hilo linapewa kipaumbele siku hiyo ya tukio.
"Kiujumla
tuko vizuri tumeunda kamati 11 na zinaongozwa na wakuu wa Wilaya, kubwa
zaidi ni kuhakikisha wanawahamasisha wananchi katika maeneo yao siku
hiyo wafike uwanjani mapema kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo,"amesema.
Huku Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Itifaki na
mapokezi Remedius Mwema amesema kuwa mpaka sasa tayari mabalozi kutoka
Nchi mbalimbali 20 wamethibitisha kushiriki katika zoezi hilo na pia
bado wanaendelea kutoa mialiko ya viongozi watakao hudhuria na wageni
kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo viongozi na wananchi
zaidi ya 140.
Amesema kuwa viongozi na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania watahudhuria uzinduzi huo sababu sensa hiyo ni yakipekee.
0 Comments