MFUMO WA KUWANASA WEZI WA MACHAPISHO WAJA

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MAKAMU  Mkuu wa chuo cha Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Profesa Emmanuel Luoga amesema Taasisi imefanikiwa kufanya utafiti na kuweza kugundua mfumo wa kubaini machapisho ya wizi (Anti-plagiarism Software) ambao utasaidia kuwanasa baadhi ya watafiti wenye tabia ya kunakili machapisho ya watafiti wengine (copy & paste.)

Prof. Luoga ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji na malengo ya chuo hicho katika mwaka wa fedha 2022/23.

Amesema kuwa chuo hicho ambacho lengo lake ni kuwa na wanasayansi na wabunifu na kukuza teknolojia katika nyanja mbalimbali ambazo zitasaidia kuwa na maendeleo endelevu kitaifa na kimataifa.

Pamoja na chuo hicho cha Nelson Mandela kubuni mfumo wa kubaini machapisho ya wizi ambao utaingizwa sokoni muda wowote wameanzisha kozi mbili muhimu katika chuo hicho ambazo ni Umahili na Ubunifu.

Makamu wa chuo akizungumzia dira ya chuo hicho ameeleza kuwa lengo ni kuwa taasisi ya kitaifa na kimataifa, uhandisi wa sayansi na teknolojia na ufanisi wa maendeleo endelevu na taaluma ya maendeleo ya viwanda na jamii.

Akizungumzia suala la vipaumbele amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2022/23 ni kujenga mabweni ya wanawake yenye kukidhi vigezo vya akina mama wenye watoto wachanga.

Sambamba na hayo Makamu wa taasisi hiyo ameeleza kuwa kwa kusirikiana na TARI wanafanya utafiti wa mbengu bora ya zao la Ndizi.

Tumeisha pata aina mbili za jamii ya ndizi ambazo zinafanyiwa utafiti katika kituo cha umahiri cha utafiti wa ndizi

Prof.Luoga. 

Aidha amesema kuwa chuo hicho kitakuwa na matumizi ya TEHAMA yenye masafa marefu kwa kuimarisha mfumo huo kwa kupata ithibati kwa kiwango cha kimataifa.

Kwa upande wa msemaji wa serikali Gerison Msigwa amesema kuwa pamoja na mambo mengine amewapongeza waandishi wa habari hususani wa kitanzania kwa kuweza kulitangaza kazi zinazofanywa na serikali.

Napenda niwaletee salamu kutoka kwa Waziri mwenye dhamana pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kwa kufanya kazi nzuri ya kutangaza kazi zinazofanywa na serikali kwa kutumia karamu zenu kizalendo.

Kazi kubwa mnayoifanya ya kuelimisha jamii ni kazi kubwa na ya kizalendo na kwa sasa kazi kubwa ya kuelezea kazi nzuri zinazofanywa na serikali zimefanikiwa"ameeleza Msigwa.

 

 

Post a Comment

0 Comments