MSD KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA NYIGINE KUINUA WAZALISHAJI WA NDANI.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA.

KATIKA kupunguza gharama za uagizaji wa Bidhaa za Afya kutoka nje ya nchi Bohari ya Dawa (MSD) imesema kuwa itashirikiana na sekta nyingine ili kuwaimarisha na kuwanyanyua wazalishaji wa ndani ya nchi.

Kwa sasa Bohari ya Dawa inaagiza zaidi ya asilimia 85 ya bidhaa za afya kutoka nje ya nchi hivyo kutumia gharama kubwa na wakati mwingine kuchelewa kupata bidhaa hizo kwa haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 17,2022 Jijini Dodoma kuhusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya Mkururugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Ali Tukai amesema kuwa maboresho yanayofanyika kwa sasa ndani ya MSD yanalenga kutekeleza majukumu yake ya msingi na kuendana na kasi kubwa ya uwekezaji wa serikali ya awamu ya sita katika sekta ya afya.

Mavere amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha 2022/2023, serikali imetenga shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kununua bidhaa za afya kwa mwaka mzima ambapo hadi kufikia mwezi Oktoba 2022, MSD imeshapokea fedha zote za robo ya mwaka ya kwanza ambayo ni shilingi Bilioni 57.

Serikali hii ya awamu ya sita imetoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za afya kwa kiwango kikubwa kupita nyakati zote ambapo mwaka wa fedha 2021/2022 serikali hii ilitoa kiasi cha Bilioni 134.9 zilitolewa na mwaka huu 2022/2023 MSD pia imetengewa kiasi cha shilingi Bilioni 200,

Mavere

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa MSD inaendelea na zoezi la usambazaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vyote vya afya vya serikali ambavyo ni 7,153 kupitia kanda zake 10 zilizowekwa kimkakati zilizopo Dodoma,Dar es salaam,Mtwara, Mwanza, Tabora, Kilimanjaro, Tanga, Kagera, Mbeya na Iringa.

MSD pia ina maduka ya jamii sita yaliyopo Mpanda (Katavi), Mount Meru (Arusha), Ruangwa(Lindi), Mbeya, Chato(Geita), na Muhimbili ambayo yanatusaidia kusogeza huduma kwa wananchi

Mavere

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya habari Maelezo Gerson Msigwa amezumgumzia Sheria ya Bima ya afya kwa wote kuwa ni nia njema ya serikali kuhakikisha kila mtanzania anapata matibabu ya aina yeyote kwa gharama yeyote na kuondokana na adha wanayokutana nayo pindi wanapokosa huduma kutokana na kukosa fedha.

Niwahakikishie kuwa nia ya serikali ni njema sana juu ya wananchi wake epukaneni na wapotoshaji ambao wanapotosha taarifa hizi juu ya hii sheria ya bima ya afya kwa wote hii ni namna nzuri ya kuhakikisha kila mtanzania anapata matibabu bila changamoto yeyote

Msigwa

Bohari ya Dawa ni Taasisi ya serikali iliyopo chini ya Wizara ya afya, iliyoundwa kwa sheria ya Bunge namba 13 ya mwaka 1993 ili kununua, kutunza na kusambaza bidhaa za afya ila kutokana na mabadiliko ya sheria ya Bohari ya Dawa, sura ya 70 iliyoidhinishwa mwezi Oktoba 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani imeiwezesha MSD kuanza kuzalisha bidhaa za afya kama jukumu lake la nyongeza kwenye majukumu yake ya msingi.

 

Post a Comment

0 Comments