NFRA YASEMA KUMEKUWA NA ONGEZEKO LA UNUNUZI WA CHAKULA


 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

AFISA Mtendaji Mkuu,Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Milton Lupa amesema kumekuwa na ongezeko la ununuzi kutoka takribani Tani 58,000 kufikia zaidi ya tani 110,000 za nafaka kwa mwaka 2021/2022.


Pia ununuzi wa nafaka kwa msimu mwaka2022/2023 unaendelea kupitia Kanda za Sumbawanga,Songea, Arusha,Shinyanga ,Makambako,Songwe na Dodoma.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma Wakati akitoa taarifa kuhusu utekekezaji wa majukumu ya NFRA katika Kipindi cha Serikali ya awamu ya sita.

Amesema ongezeko la hifadhi ya chakula imewezesha wakala kuwa na akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya kuhudumia kwa wakati mahitaji mbalimbali ya dharura au Upungufu wa chakula unaoweza kujitokeza nchini.

 

Serikali ya Rais Samia imeimarisha Hifadhi ya Chakula Nchini kwa kuongeza akiba ya chakula inayohifadhiwa na wakala kuwa zaidi ya mara mbili ya kiasi kilichokuwa kinahifadhi kipindi cha miaka mitatu ya hivi karibuni

Na kuongeza "Wakala umepata mafanikio makubwa katika Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ni nguzo imara ya kuongeza ufanisi wa NFRA katika utekelezaji wa majukumu yake," Amesema Afisa Mtendaji huyo Lupa

Aidha amesema kuwa Serikali ya awamu ya 6 imewezesha NFRA kuimarisha uchumi wa makundi mbalimbali yakiweno ya wakulima,vyama vya ushiriki,sekta binafsi na wananchi kwa ujumla kupitia mapato yanayopatikana kwa kuuza nafaka kwa NFRA hivyo kuwa na soko la uhakika kwa wakulima.

 

Ameeleza wakala umekuwa ukinunua nafaka kwa bei nzuri hivyo kuwa soko tegemezi kwa wakulima wengi na kuwapa motisha wakulima kujishughulisha na Kilimo.

Jukumu kuu la NFRA ni kuihakikisha Nchi usalama wa chakula kwa kununua na kuhifadhi akiba ya chakula na kutoa chakula Cha msaada kwa waathirika waliokubwa na majanga mbalimbali ya kitaifa,Aidha wakala huzungusha akiba ya chakula kwa lengo la kutoa la nafasi ya uhifadhi na kuingiza mapato ya kununua akiba mpya ya chakula,Mazao yanayonunuliwa na kuhifadhiwa kwa sasa ni mahindi,mtama na mpunga.


Post a Comment

0 Comments