SERIKALI IMETOA BILION 46.89 KULIPA WATUMISHI WALIOONDOLEWA KAZINI VYETI FEKI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SERIKALI imetoa jumla ya shilingi Bilioni 46.8 9 kwaajili ya kuwalipa Watumishi walioondoleewa kazini kwa vyeti feki 

Malipo hayo ni makato ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo NSSF ni asilimia 10, pamoja na PSSF asilimia 5.

Akizungumza Jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira, na wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amesema RAIS Samia ameridhia watumishi hao walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti kurejeshewa michango yao waliyokatwa kwenye mishahara na kuwasilishwa kwenye mifuko ya jamii.

Wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei mosi Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA) kupitia risala yao waliwasilishwa ombi kwa Mheshimiwa Rais aangalie namna ya kuwafuta jasho watumishi hao. Rais alielekeza kufanyika kwa uchambuzi Ili kuona namna gani Serikali inaweza kuhitimisha suala hilo,

Kufuatia uchambuzi uliofanyika Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa watumishi wote walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti warejeshewe michango yao tuu waliyokatwa kwenye mishahara na kuwasilishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na kufuatia maelekezo hayo mifuko ya hifadhi ya jamii PSSF na NSSF itarejesha michango ya wafanyakazi iliyowasilishwa kwenye mifuko hiyo bila kuhusisha michango ya mwajiri

Prof.Ndalichako

Aidha akizungumzia kuhusu watumishi waliofariki na wanapaswa kurejeshewa michango yao Profesa Ndalichako amesema wapo watu walioandikwa kwenye mirathi hao ndio watakaostahili kupatiwa fedha hizo.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama ameagiza waajiri wote wa mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanazingatia maadili ya utumishi wa Umma na kuhakikisha kuwa kusiwe na mianya yoyote ya rushwa na kusema kuwa zoezi hilo ni haki ya watumishi hao walioondolewa kazini

Waajiri wote Mamlaka za Serikali za Mitaa wanatakiwa kufanya mambo yafuatayo, tunaagiza wawajibike katika kutoa ushirikiano na watakaohusika na zoezi hili la watumishi,wahahakikishe wanaandaa madawati ya msaada. Kuna watu wanakuwa hawajui wakifika waende wapi

Waajiri  wahakikishe wanazingatia misingi ya utumishi wa umma na Utawala Bora katika zoezi hili kwani wale watumishi ni haki yao hawatakiwi kuipata kwa bugudha yoyote tunaamini waajiri wataifanya kazi hii kwa weledi na uadilifu hatutarajii zoezi hili kuwa mradi kwa baadhi, na TAKUKURU kuanzia sasa wahahakikishe wanazingatia pasiwe na mianya ya rushwa

Hata hivyo amesema waajiri ndio waliosimamia zoezi la kuwaondoa kazini hivyo wanauwezo kwakuwa nyaraka zote wanazo.

Ikumbukwe kuwa malipo hayo yanakuja baada ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kupitia risala yao wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi kumuomba Rais Samia aangalie namna ya kuwafuta jasho watumishi hao walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti.

 

Post a Comment

0 Comments