SERIKALI IMEWATOA HOFU WATUMIAJI WA NYAMA YA NGURUWE KUWA NI SALAMA KABISA.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SERIKALI imewatoa hofu watumiaji wa nyama ya Nguruwe maarufu (Kitimoto) na kueleza kuwa nyama yake ni salama kama ilivyo nyama ya wanyama wengine.

Hayo yameelezwa hii Leo jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dk.Stella Bitanyi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo juu ya utekelezaji wa shughuli za Wakala katika mwaka wa fedha 2022/23.

Ametoa kauli hiyo kutokana na kuwepo na mkanganyiko wa maneno kuwa mnyama huyo si salama kwa kuliwa kutokana na kile ambacho walikuwa wakieleza kuwa Nguruwe ana wadudu wengi na hafai kuliwa.

Akitoa ufafanuzi Dk.Bitanyi amesema kuwa nyama ya Nguruwe ni salama kama ilivyo nyama ya wanyama wengine isipokuwa kinachotakiwa ni kuhakikisha mnyama huyo anapatiwa chanjo na dawa kama inavyotakiwa.

Nyama ya Nguruwe ni salama kabisa kama ilivyo nyama ya wanyama wengine kinachotakiwa ni kupatiwa tiba na chanjo zinazotakiwa, Nguruwe ana minyoo ambayo ni mibaya endapo utaila inakuwa na tabia ya kuingia kwenye ubongo ambao unaweza kuvuruga ubongo

Dk.Bitanyi.

Aidha amesema kuwa shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania kupitia programu inayofadhiliwa na umoja wa Ulaya inayoitwa Agri Connect imezindua kampeni ya kitaifa ya lishe Bora ambayo ni mtaji ili kujenga tabia zinazofaa za milo Nchini Tanzania kwa kutumia vyakula vinavyopatikana Nchini.

Pia amesema katika kampeni hiyo suala zima la Sumukuvu linalengwa kwa sababu katika vyakula vinavyopatikana hapa Nchini ni jambo mojawapo linalochangia katika masuala ya usalama wa chakula.

Chakula salama ni muhimu kwa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu,wakati chakula si salama, huathiri vibaya usalama wetu wa chakula na lishe, afya, makuzi ya watoto, na uwezo wa watu wazima kuongoza kwa tija maisha.

Dkt Bitanyi. 

Hata hivyo amefafanua kuwa Usalama wa chakula una athari kubwa kwa biashara na uchumi, Makadirio ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa chakula kisicho salama hugharimu uchumi wa chini na wa kati karibu dola za Kimarekani bilioni 95 katika uzalishaji unaopotea kila mwaka

Mycotoxins ni misombo inayozalishwa na ukungu ambayo kwa kawaida hupatikana kwenye udongo na inaweza kuchafua mazao bidhaa kama vile nafaka (mahindi, mtama) na nafaka nyingine shambani au baada ya kuvuna.

 

Post a Comment

0 Comments