SERIKALI IMEWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WADAU WA FILAMU KUJIAJIRI

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

KATIBU Mtendaji Bodi ya filamu Tanzania Dkt Kiagho Kilonzo amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wadau wa Filamu kujiajiri, hivyo kuongeza na kukuza pato la Taifa, kupunguza umaskini na kuchochea maendeleo ya Sekta nyingine mtambuka kama vile Utalii. 

Akiongea na waandishi Jijini Dodoma Wakati akieleza utekekezaji wa majukumu amesema hadi sasa kamati imeshapokea malalamiko 30 na kuyashughulikia, ambapo takriban shilingi milioni 300 zilizokuwa zimedhulumiwa zimesharejeshwa kwa wasanii.

Amesema Bodi hiyo inaratibu Kamati Maalum ya kutetea haki za Wasanii iliyoundwa na Waziri mwenye dhamana Mohamed Mchengerwa lengo likiwa ni kusimamia masuala ya Sanaa nchini na upatikanaji wa haki kwa wasanii.

Aidha amesema Malalamiko 22 yamesuluhishwa, na Malalamiko 8 yapo katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa. 

Amesema baadhi ya malalamiko yaliyopokelewa na kushughulikiwa ni yale ya marehemu Amri Athumani (King Majuto), Marehemu Steven Kanumba, Msanii David Ganzi (Young Dee), Mzalishaji wa Tamthilya Samwel Isike

Ameeleza Bodi imeunda Kamati maalum ya kurudisha utamaduni wa kutazama filamu katika Kumbi za Sinema hatua hiyo inatarajiwa pia kutoa mchango stahiki katika uchumi wa wadau wa Sekta na Taifa kupitia viingilio vya mlangoni. 

Amesema kwa kipindi cha Januari hadi Disemba, 2021 pekee inakadiriwa kuwa ilichangia takriban ajira 30,000 zilizotokana na Filamu (waigizaji, waandaaji na watoa huduma). 

Kwa mazingira ya Kitanzania, Filamu moja (wastani wa watu 20, tamthilia moja wastani wa watu 1000,

Kiasi hicho ni ongezeko la nafasi 5,000 kutoka 25,000 kiasi kinachokadiriwa kuzalishwa mwaka 2020. 

Kwa Upande wake Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Bodi ya Filamu ni Kati ya nyenzo inayotumika katika kutangaza nchi kwa kupitia Filamu za wasanii hivyo basi Wasanii hawana budi kutembea kifua mbele kwani sanaa ndio kitu kinachoitangaza nchi .



 

 

Post a Comment

0 Comments