SERIKALI KUANZISHA PROGRAM YA UANDAAJI FILAMU ZENYE MAUDHUI YA KUTANGAZA NCHI.

📌RHODA SIMBA

SERIKALI inatarajia kuanzisha program ya kuratibu uandaaji wa filamu zenye maudhui ya kutangaza utajiri wa nchi katika eneo la utamaduni, historia na jiografia yake.

Aidha, amesema hadi sasa Kamati ya kutetea Haki za Wasanii imeshapokea malalamiko 30 na kuyashughulikia, huku takribani sh. milioni 300 zilizokuwa zimedhulumiwa zimesharejeshwa kwa wasanii.

Hayo yamesemwa leo October 04 Jijini Dodoma, na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Dk. Kiagho Kilonzo wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli za bodi na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu wa fedha.

Amesema lengo la filamu hiyo ni kujenga mapenzi hasa kwa vijana wa kitanzania kwa nchi yao kwa kuwaongezea ufahamu wa rasilimali waliyonayo.

Programu hii itasaidia kutunza kumbukumbu za kihistoria kwa kuhusisha taarifa za viongozi wetu mbalimbali waliofanya mambo makubwa kama vile Mwl. Julius Nyerere ambaye alisaidia ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika

Kuhusu haki na maslahi ya wasanii Dk. Kilonzo amesema TFB inaratibu kamati maalum ya kutetea haki za wasanii iliyoundwa na Waziri mwenye dhamana ya kusimamia maswala ya sanaa nchini kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na kuhuishwa tena 2019 na 2020 itakayodumu hadi mwishoni mwa mwaka 2022.

Amesema hadi sasa Kamati imeshapokea malalamiko 30 na kuyashughulikia, ambapo takriban sh. milioni 300 zilizokuwa zimedhulumiwa zimesharejeshwa kwa wasanii:

Malalamiko 22 yamesuluhishwa, na malalamiko nane yapo katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa baadhi ya malalamiko yaliyopokelewa na kushughulikiwa ni yale ya marehemu Amri Athumani (King Majuto), marehemu Steven Kanumba, Msani David Ganzi (Young Dee), Mzalishaji wa Tamthilya Samwel Isike ambayo yalitokana na kuingia mikataba mibovu.

Katika hatua nyingine Dk. Kilonzo amesema TFB imeendelea kuongeza wigo wa utoaji ajira ambapo kwa kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka jana inakadiriwa kuwa ilichangia takriban ajira 30,000 zilizotokana na Filamu.

Amesema kwa mazingira ya Kitanzania, Filamu moja inakuwa na wastani wa watu 20, tamthilya moja wastani wa watu 100).

Kiasi hicho ni ongezeko la nafasi 5,000 kutoka 25,000 kiasi kinachokadiriwa kuzalishwa mwaka 2020 hadi kufikia ajira 30000 ambazo zimezalishwa mwaka jana na kwa mwaka huu tunatarajia takwimu hizo kuongezeka kwa wingi kwasababu tasnia imekuwa

 


Post a Comment

0 Comments