SERIKALI KUWEKA MIKAKATI YA KUONGEZA UZALISHAJI WA SUKARI NCHINI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SERIKALI imesema imeweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani laki 380,000 inayozalishwa sasa nchini hadi Tani laki 756,000 ifikapo mwaka 2025.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari nchini Prof.Kenneth Bengesi wakati  akielezea muelekeo wa Taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023.

Mpango wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kwamba mpaka ifikapo mwaka 2025 /2026 nchi inakuwa na sukari ya kutoshaa pamoja na ongezeko la viwanda vya kuzalisha sukari.

Amesema miaka ya nyuma nchi ilikuwa inaagiza sukari mpaka tani 183,000 lakini Serikali imefanya juhudi ambapo kwa sasa imepunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi kutoka tani 144,000 mwaka 2017 hadi tani 50,000 kufikia Juni, 2022.

Nchi hii tangu ipate Uhuru, ndio tumepata wawekezaji katika upande wa sukari ikiwemo kiwanda cha Sukari Bagamoyo na cha Mkulazi kinachotarajiwa kuanza mwaka 2023, kuna upanuzi mkubwa wa kiwanda cha Kilombero kitakachokuwa na uwezo wa kuongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani 130,000 hadi kufikia tani 271,000

Pia amesema uwekezaji wa kiwanda cha Sukari cha Kilombero ni zaidi ya bil. 500 ambapo Serikali ina asilimia 25 ya hisa katika kiwanda hicho,lakini pia kiwanda cha Sukari cha Kagera kuna upanuzi mkubwa sana umefanyika ambapo kwa sasa kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani 140,000, ifikapo 2025/26 kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 170,000.

Kiwanda cha Sukari Mtibwa kinatarajia kuongeza uzalishaji kutoka tani 48,000 za sasa hadi tani 100,000 ifikapo mwaka 2025/26, TPC kwa sasa inazalisha tani 100,008 na wana uwezo wa kufikia tani 120,000, na kiwanda cha Manyara kinazalisha tani 8,000 kwa sasa na kinatarajiwa kuzalisha tani 10,000 kwa mwaka 2025/26

 Kupitia viwanda vya ndani ya nchi, tunao uwezo wa kuzalisha tani 380,000 za sukari kwa ajili ya matumizi ya nyumbani lakini sukari kwa ajili ya matumizi ya viwandani bado haijaanza kuzalishwa nchini.

Serikali ya Awamu ya Sita imeweka msukumo mkubwa na mazingira mazuri katika kuhakikisha tunaelekea kuzalisha sukari ya matumizi ya viwanda, tayari kuna wawekezaji wameshaanza kuonesha nia kwenye eneo hilo”amesema Bengesi.

Wakati huo huo amesema kuwa takwimu zinazoishia Juni, 2022, mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida yaliyotumika kwa mwaka mzima ni tani 440,000 na sukari ya matumizi ya viwanda iliyoagizwa kutoka nje ni tani 205,000.

Mwaka 2012/13, uzalishaji wa sukari ulikuwa tani 293,000 na kwa sasa uzalishaji ni tani 380,000, ni vyema kuendelea kuzalisha sukari ndani ya nchi kwa ajili ya kulinda usalama wa sukari tunayoitumia na kutengeneza ajira kwa wananchi

 

 

Post a Comment

0 Comments