TANROADS: TUTAENDELEA KUDHIBITI UZITO WA MAGARI BARABARANI

 

 


 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) umesema utaendelea kudhibiti uzito wa magari barabarani ili kuzilinda barabara zilizopo kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini hapa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila amesema licha ya kulinda barabara hizo,wataendelea kulinda hifadhi za barabara.

Akizungumzia utekelezaji wa bajeti ya taasisi hiyo na mwelekeo katika mwaka huu wa fedha Mhandisi Mativila alisema kwa sasa wanaendelea kuratibu na kusimamia, ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara kuu na za Mikoa zenye urefu wa kilometa 36,362.

Amesema hadi kufikia Juni mwaka huu mtandao wa barabara zenye lami ulikuwa umefikia kilometa 11,513.

TANROADS inaendelea kudhibiti uzito wa magari barabarani na kulinda maeneo ya hifadhi ya barabara ambapo hadi sasa ina mizani 70 ya kudumu, 22 ya kuhamishika na mizani 15

Mhandisi Mativila


UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya mendeleo Mhandisi Mativila amesema miradi 14 yenye urefu wa kilometa 883 imekamilika kati ya Aprili 2021 hadi sasa ambayo imegharimu sh. Trilioni 1.37. 

Ametaja miradi hiyo kuwa ni barabara ya Kidahwe hadi Kasulu yenye urefu WA kilometa 63, barabara ya Nyakanazi hadi Kibondo kilometa 50 
Mbinga hadi Mbamba Bay kilometa 66 
Njombe hadi Moronga kilometa 53.9), 
Moronga hadi Makete kilometa 53.30.

Ametaja barabara nyingine zilizokamilika kuwa ni ya Makutano hadi Natta kilometa 50 Mkoa, Kikusya Ipinda Matema kilometa 39.10 Chunya Makongolosi Kilometa 39.

"Miradi ya madaraja makubwa .manne iliyokamilika ni pamoja na daraja la Tanzanite, Ruhuhu, Magara, Mara ,Msingi , Singida ,Sibiti na daraja la Wami,"ametaja

Ameongeza kuwa "Miradi mitatu ya madaraja makubwa ipo katika hatua mbalimbali ya utekelezaji kwa kwa gharama ya sh.bilioni 701 miradi hiyo ni daraja la J. P. Magufuli Kigongo Busisi km 3.2 (Mwanza) ,Pangani (m 520) Kitengule (m 140).

Mhandisi amesema serikali imekamilisha usanifu wa kina wa madaraja makubwa sita ambayo yanasubiri kuanza utekelezaji wake.

 

Madaraja hayo ni pamoja na daraja la Simiyu katika barabara ya Mwanza Musoma, Bwawa la Mtera katika barabara ya Iringa Dodoma, daraja la 
Mzinga katika barabara ya Dar es Salaam Kibiti, Mitomoni Ruvuma Mkenda Ruvuma, na daraja la Jangwani.

 MIRADI YA BARABARA.

Mhandisi Mativila amesema serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ambapo miradi 44 ya barabara yenye urefu wa kilometa 1,523 na gharama ya she. trilioni 3.8 ipo katika hatua mbali mbali ya ujenzi nchi nzima. 

Amesema kwa mwaka wa fedha ulioishia , kati ya Julai 2021 hadi Mei jumla ya mikataba 20 inayohusisha miradi ya ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege inayogharimiwa moja kwa moja na fedha za ndani na mingine kugharimiwa kwa fedha za washirika wa maendeleo ilisainiwa.

Amesema mikataba ya ujenzi wa barabara zenye jumla ya km 582.455 imesainiwa na mikataba ya ujenzi wa kiwanja cha ndege msalato na kumalizia jengo la Kiwanja cha ndege Songwe pamoja na mizani ya Rubana ilisainiwa. 

"Gharama ya miradi yote 20 ni sh. bilioni 1,460.84 ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji,"amefafanua

Post a Comment

0 Comments