📌PASCHAL NKWABI
Watanzania wametakiwa kuchagua na kujisomea vitabu vyenye maudhui yanayokuza maarifa ili kuondokana na vikwazo vya umaskini na ujinga sanjari na kutumia maarifa hayo kuleta mabadiliko miongoni mwa jamii
Rai
hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa kitabu cha ukombozi kutoka
kitabuni chenye maudhui ya dini na maisha ya kwaida.
Mstahiki
Meya wa Halmashuri ya Jiji la Dodoma Prof: Device Mwamfupe kwa niaba ya Naibu
Waziri Wizara ya Kilimo Anthony Mavunde ambapo mara baada ya uzinduzi huo
amesema itakuwa na manufaa kwa watoto hasa kumtambua Mungu.
Amesema
kuwa uzinduzi wa vitabu si kitendo cha kukata utepe pekee kuashiria tendo
husika, lakini uzinduzi halisi ni ile hali ya kukipata kitabu chenyewe kukisoma
na kutumia maarifa yaliomo kwenye kitabu hicho kwa lengo la kujiletea mabadiliko
chanya kwenye maisha.
Profesa
Mwanfupe ameeleza kuwa binadamu ana
minyororo mingi ikiwemo ya ujinga, kutawaliwa na watu wengine na dhambi, hata hivyo amesema kuwa
mnyororo mkubwa ni wa kutofahamu au kuwa
mjinga akitoa mfano wa mtu kukasirika na kujinyonga kwenye tawi la mpampai
kuonesha hali ya kutojua hata namna
mjinga asiyeweza kuamua hata
kwenye uamuzi wa kijinga.
Amesema
kuwa minyororo hiyo inaweza kufunguliwa kwa kutumia maarifa hasa ya
kujisomea akitumia muktadha wa uzinduzi
wa kitabu hicho kuwa Mungu ni chanzo cha
kiu ya kuondokana na minyororo hiyo.
Kuhusu
kusoma amewataka wazazi kuchagua vitabu vizuri vinavyoweza kuwafanya watoto wao
kuongeza maarifa zaidi ikiwemo kuchagua vipindi vya Runinga pamoja na sinema
zenye kukuza ujuzi chanya na sio za mauaji au mapigano.
Amewakumbusha
watanzania kutonunua vitabu na kuviweka maktaba kwenye nyumba zao kwa mkumbo
akimanisha kutozitumia kujisomea au kusoma vitabu wanavyonunua akiwataka
kuzitumia maktaba hizo kusoma.
Bwana
Maneno Mung’ong’o ambaye ni mtunzi na mwandishi wa kitabu hicho amesema kuwa ameandika
na kuzindua kitabu hicho ili kuamsha ari ya usomaji, ununuzi na utunzaji wa
vitabu, utamaduni unaoonekana kutoweka kila uchwapo hapa nchini.
Kwenye
maelezo yake bwana Mugo’ng’o amesema kuwa katika uzoefu wake amegundua kuwa,
wasomaji wa vitabu ni wachache, licha ya mabadilko ya uboreshaji wa nyumba nyingi hazina maktaba ,na wazazi
kutowaononesha watoto wao ari ya kujisomea vitabu.
Ameonya
kuwa hali hiyo ni hatari hasa kwenye dunia hii ya ushindani yenye ukosefu wa ajira ambayo inataka jamii isome
vitabu vya kutosha kuongeza maarifa ili kukuza ujuzi wa kupambana na mzingira
pamoja na kuleta maendeleo chanya.
Ameshauri
wazazi na shule kukuza mifumo ya utunzaji wa vitabu kwa lengo la kusomwa na
wanzafunzi akisema, itasaidia kizazi cha sasa kupenda kujisomea, yeye binafsi
akiahidi kuanzisha klabu za usomaji wa vitabu
Miongoni
mwa watu walioalikwa na kuhudhuria uzinduzi huo ni Bwana Francis Mlelwa alipozungumzia
juu kitabu hicho amesema baada ya kusoma
kitabu hicho amegundua kuwa kuna mambo mengine mtu anaweza kutojua asiposoma
lakini akisoma huenda anaweza kujua mengi zaidi .
Uandishi
na vitabu bado ni utumaduni muhimu sana kwenye
kuongeza maarifa ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hasa unapotumika kuleta
mabadiliko chanya miongoni mwa jamii.
0 Comments