HALMASHAURI ya Wilaya ya Chamwino kupitia Mkuu wa Idara ya Ardhi Enock Mligo imeishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa kiasi cha fedha cha shilingi milioni mia tatu kwaajili ya zoezi la kupanga na kupima viwanja mia nne hamsini.
Akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma Mligo amewakaribisha wawekezaji wanaotaka kuwekeza Wilaya ya Chamwino kununua viwanja hivyo ambavyo vimeanza kuuzwa kuanzia leo Oktoba 25.
Naomba nitumie nafasi hii pia kuipongeza serikali kwa kutupatia milioni 300 kwaajili ya kupanga na kupima viwanja hivi ambavyo vimekamilika kwa upimaji vimeidhinishwa michoro yake na vipo tayari kuombwa natumia nafasi hii kuwakaribisha wananchi, wawekezaji na wafanyakazi wote waje wanunue viwanja hivi
Enock Mligo
Awali akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Dk. Semistatus Mashimba amesema Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha shilingi bilioni ishirini na tatu kwaajili ya miradi mbalimbali kama vile kilimo ujenzi wa bwawa la umwagiliaji, na shule ya mfano
Tuna hospitali kubwa ya Fistula itajengwa hapa na kutoa huduma mbalimbali itakuwa kilometa 7 tu kutoka hapa Chamwino Mjini,Chamwino panaenda kuboreshwa hapa maeneo ya kuzunguka Ikulu patakuwa na mpangilio mzuri wa mashamba ya mjini, eneo tutakalo panga tutakuwa na barabara tatu za mzunguko (round about) na patakuwa pazuri mno
Dk Mashimba.
Akizungumza kuhusu baadhi ya watu wanaonunua maeneo na hawayaendelezi DK Mashimba amesema wamepanga na wameweweka sheria ndogo kwa mtu ataye nunua ndani ya mwaka mmoja au mwaka mmoja na nusu anapaswa awe ameanza kupaendeleza kutokana na maeneo hayo kuwa karibu na Ikulu hivyo wanahitajika watu watakaofanya uwekezaji wa haraka.
0 Comments