BILION 118.8 KUBORESHA HUDUMA ZA MELI NCHINI

 


📌RHODA SIMBA  

MKURUGENZI wa kampuni ya huduma za meli Erick Hamisi amesema katika kutekeleza miradi mbalimbali na kuboresha huduma za usafirishaji kwa njia ya maji serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 118.8 kwaajili ya utekelezaji wa miradi 12 ambapo miradi minne ni miradi mipya.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu kampuni ya huduma za meli na vipaumbele vya mwaka wa fedha 2022/ 2023 hamisi alisema miradi mitano ni ukarababati wa meli na mitatu ni miradi inayoendelea kukalimishwa ikiwemo meli ya mv mwanza hapa kazi tu ambapo bilioni 53.9 zitatumika kurabati miradi ya ziwa tanganyika.

‘’Kama nilivosema ziwa Tanganyika hakuna meli inayofanyakazi mpaka sasa  lakini tunafahamu fursa ambazo zipokatika ziwa Tanganyika lakini ukuachana ukweli kwamba tunapakana nanchi ambayo inaidadi kubwa ya watu lakini rasilimali kubwa ya misitu na madini drc kongo na hata Zambia pia sasa serikali ya awamu ya sita imeamua kuwekeza kwa kiwango kikubwa sana katika ziwa Tanganyika billion 53.9 Ambazo miradi ya huko tutajenga chelezo meli mpya ya abiria 600 na tani 400 za mizigo na mradi wa tatu ziwa Tanganyika ni ujenzi wa meli mpya ya mizigo tu,’’amesema.


 

Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa mradi mwingine ni ujenzi wa meli mpya ya abiria 600 na tani mia nne za mizigo ambapo tayari fedha zimetolewa kiasi cha shilingi bilioni 12 kwaajili ya awamu ya kwanza, ukarabati meli ya sangara, na ukarabati meli ya mv liemba huku akibainisha dhamira ya taasisi hiyo katika kukuza utalii.

"Nitumie fursa hii kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi cha Shilingi 111,894,892,622 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwaajili ya kutekeleza miradi 12 kwa hatua tofauti ambayo minne kati ya hiyo ni mipya, mitano ni ya Ukarabati itakayoanza mwaka wa fedha 2022/2023 na mitatu ni ile inayoendelea ya MV Mwanza, MV Umoja pamoja na MT. Sangara,

Kati ya fedha hizo kiasi cha Shilingi 53,969,470,567 ni kwa ajili ya kutekeleza miradi saba katika mkoa wa Kigoma na Kiasi cha Shilingi 57,925,422,055 ni kwaajili ya kutekeleza miradi mitano katika mkoa wa Mwanza


Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali ya awamu ya sita mbali nakufanya juhudi za miradi ya ujenzi wa meli serikali pia inafanya maboreshaji wa bandari zote za maziwa makuu.

"Kunakazi kubwa inayoendelea tumeambiwa kuhusu chelezo ya mwanza,chelezo kigombo kubwa kabisa inayoenda kufanyika pale ya Tani 500 lakini tunaujenzi ambao umekamilika kwenye bandari yetu ya karema asilimia 100 bandari ya kimkakati kabisa na pia Juzi tumeona Mheshimiwa Rais ameweka jiwe la msingi kwenye kuboresha bandari zile za kibirizi na ujiji kigoma,"amesema Msigwa.

Kampuni ya huduma za meli tanzania inawajibu wa kutoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo kwanjia ya maji ambapo inamiliki vyombo 18 ambapo meli ni 17 na boti 1 ya utalii.

 

Post a Comment

0 Comments