MISA TAN YAENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI KUHUSU UHURU WA KUJIELEZA



📌MWANDISHI WETU

TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania (MISA-TAN) imeendesha mafunzo ya siku (3) ya  kuwajengea uwezo wa kutafuta na kuchakata habari zitakazo chochea Uhuru wa kujieleza kwa Wanahabari zaidi ya 40 kutoka Mikoa ya Tabora, Dodoma, Shinyanga, Simiyu na wenyeji mkoa wa  Singida.

Mafunzo hayo yameandaliwa na MISA TAN kwa ufadhili wa Ubalozi wa Kanada nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo mwishoni mwa wiki, Andrew Marawiti kutoka Misa-Tan, amesema  lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuzalisha maudhui yenye ubora yanayohusiana na Uhuru wa Kujieleza.


MISA TAN inatamani kuona vyombo vya habari vinatoa kipaumbele kuandaa maudhui yatakayochochea Uhuru wa Kujieleza ili tutengeneze jamii ambayo sauti ya kila mmoja iwe na uwezo wa kusikika.

Kwa upande wake Mwezeshaji wa Mafunzo hayo mwandishi mkongwe Marko Gideon, amewataka Wanahabari  kutumia kalamu zao vyema kuandika habari za uhuru wa kujieleza katika nyanja mbalimbali ili kupaza sauti za wananchi ambao kwa kiasi kikubwa wanategemea vyombo vya habari kufikisha vilio vyao. 



Bw.Gideon amesema kwamba Uhuru wa Kujieleza ni moja ya nguzo katika kujenga msingi imara Utawala wa bora kwa vile wananchi wote watashiriki katika kutoa maoni kwa ujenzi wa mambo mbalimbali katika taifa.


“Nchi isiyo na Uhuru wa kujieleza hautakuwepo uwajibikaji kwa viongozi, hakutakuwa na usawa wa kisheria, hakuna uwazi, uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki, wala kudhibiti matumizi mabaya madaraka kwa viongozi, " amesema 

Mwamvita Issa mmoja wa Washiriki

 

Nao baadhi ya washiriki wameishukuru MISA TAN kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yamewasidia kupata maarifa yatakayowawezesha kuandaa maudhui bora katika vyombo vyao vya habari.

“Mafunzo yamenijengea uwezo na nimepata maarifa kuhusu vile ninavyoweza kubainisha vyanzo vyangu ili habari yangu iweze kuleta mabadiliko katika jamii.” Amesema Mwamvita Issa mshiriki kutoka mkoa wa Shinyanga.





Post a Comment

0 Comments